If you need it, we can provide: • USA 24 hours Passport service • Rush and emergency USA passport • Expedited Visa process for U.S. & foreign countries • Document Authentication •Document Legalization..For more information please contact us at: 703-286-7713

http://swahilivilla.blogspot.com/2014/01/mahojiano-na-faria-zam-kuhusu-msaada-wa.htmlKwa kuchangia chochote kile alichonacho kupitia Hilmy Disability Charity Organisation. Wasiliana na Mkurugezi wa Hilmy Disability Charity Organisation. Faria Zam. kwa UK Number ya Simu. 745-501-4372 Au Abou Shatry. U.S.A No' 301-728-3977

 http://www.dickysmallsauto.com/

DICK SMALLS AUTO MOTIVE WE CAN HANDLE ALL OF YOUR REPAIR AND SERVICE NEEDS INCLUDING CALL US NOW!(301) 931-3300. 10111B BACOCON DRIVE,BELTSVILLE,MD 20705

Wednesday, April 5, 2017

KENYA: BEI YA UNGA ITASHUKANa ELVIS ONDIEK

SERIKALI imesema bei ya unga wa mahindi itapungua hadi Sh115 wiki ijayo, katika juhudi za kupunguzia Wakenya gharama ya maisha ambayo imekuwa ikizidi kupanda.

Duka
Mhudumu katika duka la jumla La Samrat mjini Nyeri akipanga pakiti za unga kwenye rafu awali. Picha/MAKTABA

Tangazo hilo lililotolewa Jumanne lilitokana na jinsi bei ya mfuko wa kilo mbili ya unga ilivyopanda hadi Sh150 katika baadhi ya maduka baada ya makadirio ya bajeti kusomwa wiki iliyopita.

Ufichuzi kuhusu jinsi bei ilivyopanda ghafla kwa kiwango cha kuvunja historia ulifanywa kwenye ripoti ya kipekee ya 'Taifa Leo’ mnamo Jumatatu.

Bajeti iliyosomwa bungeni na Waziri wa Fedha Bw Henry Rotich ilikuwa imeeleza mikakati itakayosaidia kupunguza bei ya unga, lakini wananchi wakashangaa kupata bei ilipanda zaidi siku chache baadaye.

Kwenye kikao cha wanahabari Nairobi baada ya kukutana na wawakilishi wa Chama cha Wasagaji wa Nafaka nchini, Bw Rotich alisema walikubaliana kuweka mikakati zaidi ili bei ya unga ipunguzwe mara moja hata bajeti inaposubiri kutekelezwa.

Kulingana naye, inatarajiwa bei ya kupakia unga, bei ya kawi na uchukuzi zipungue mara moja, na pia mahindi yaliyohifadhiwa na Bodi ya Kitaifa ya Uzalishaji wa Nafaka (NCPB) yatolewe kwa wasagaji wa nafaka mara moja.

Magunia karibu milioni moja ya mahindi kutoka NCPB yatasaidia kupunguza bei ya unga huku yale yatakayoagizwa kutoka kwa mataifa ya nje bila kutozwa ushuru yakisubiriwa.


“Tunatarajia bei ya unga itazidi kupungua kadri na jinsi siku zinavyozidi kusonga, hasa baada ya mahindi yatakayoagizwa kutoka mataifa ya nje kuwasili nchini,” akasema.

Waziri wa Kilimo Bw Willy Bett ambaye pia alikuwa katika kikao hicho cha wanahabari alisema uhaba wa mahindi umekumba ukanda wote wa Afrika Mashariki na si Kenya pekee inakabiliwa na tatizo hilo.

Kulingana naye, mikakati inayochukuliwa na serikali itasaidia pakubwa kuleta afueni kwa wananchi.

“Hatua tunayochukua sasa ni kutoa magunia karibu milioni moja ya mahindi tuliyohifadhi kusaidia wakati wa dharura. Hii ni hatua tutakayochukua mara moja kuanzia kesho,” alisema.

Aliongeza huenda wasagaji wa nafaka wakahitaji kati ya siku nne au tano kusafirisha mahindi hayo kutoka kwa maghala ya NCPB ndiposa inatarajiwa bei ya unga itapungua baada ya wiki moja.

No comments:

Post a Comment

Maoni yako