If you need it, we can provide: • USA 24 hours Passport service • Rush and emergency USA passport • Expedited Visa process for U.S. & foreign countries • Document Authentication •Document Legalization..For more information please contact us at: 703-286-7713

http://swahilivilla.blogspot.com/2014/01/mahojiano-na-faria-zam-kuhusu-msaada-wa.htmlKwa kuchangia chochote kile alichonacho kupitia Hilmy Disability Charity Organisation. Wasiliana na Mkurugezi wa Hilmy Disability Charity Organisation. Faria Zam. kwa UK Number ya Simu. 745-501-4372 Au Abou Shatry. U.S.A No' 301-728-3977

 http://www.dickysmallsauto.com/

DICK SMALLS AUTO MOTIVE WE CAN HANDLE ALL OF YOUR REPAIR AND SERVICE NEEDS INCLUDING CALL US NOW!(301) 931-3300. 10111B BACOCON DRIVE,BELTSVILLE,MD 20705


Tuesday, April 25, 2017

KENYA: DENNIS WAWERU AMENUNULIA WAHUNI MAGODORO KUVURUGA MCHUJO - WAPINZANI

Na LEONARD ONYANGO

JOTO la kura za mchujo za chama cha Jubilee jijini Nairobi linazidi kupanda huku wawaniaji wa eneobunge la Dagoretti Kusini wakishutumu mbunge wa eneo hilo Dennis Waweru kwa kukodisha wahuni kuvuruga kura za mchujo zitakazofanyika Jumatano.

Dennis Waweru
Mbunge wa Dagoretti Kusini Dennis Waweru. Picha/WILLIAM OERI

Wawaniaji wa ubunge John Kiarie, Gaciku Muhu, Dkt Njoki Ndiba na Njogu wa Nguo; na wagombeaji 15 wa udiwani katika eneobunge hilo, Jumapili walidai kuwa Bw Waweru ameficha wahuni katika Jumba la CDF la Dagoretti Kusini.

Wawaniaji hao walidai kuwa wana ushahidi kwamba Bw Waweru amenunua magodoro yanayolaliwa na wahuni hao katika jumba la CDF.

“Bw Waweru amenunua magodoro yanayotumiwa na wahuni katika jumba la CDF. Wahuni hao wanaandaliwa kuzua rabsha wakati wa kura za mchujo Jumatano,” akasema Bw Kiarie.

Wawaniaji hao pia wanataka Bodi ya Uchaguzi ya Jubilee inayoongozwa na Andrew Musangi kufutilia mbali jina la Bw Waweru kutoka katika orodha ya wawaniaji kutokana na madai kwamba amekuwa akizua vurugu na kutishia wapinzani wake.

Lakini Bw Waweru alipuuzilia mbali madai hayo huku akikiri kuwa kuna magodoro 20 katika jumba la CDF la Dagoretti. Lakini alisema lengo la magodoro hayo ni kusaidia waathiriwa wa mikasa ya moto.


“Ni kweli kuna magodoro katika afisi za CDF lakini si ya kulaliwa na wahuni kama wanavyodai wapinzani wangu. Magodoro hayo pamoja na mablanketi yalinunuliwa na afisi ya CDF ili kusaidia wahanga wa mikasa ya moto ambayo imekuwa ikishuhudiwa mara kwa mara katika eneobunge langu,” Bw Waweru akaambia Taifa Leo.

Bw Waweru alisema madai hayo ni ishara kwamba wapinzani wake wameanza kuhisi kushindwa katika kura za mchujo za Jumatano.

Chanzo: swahilihub.com

No comments:

Post a Comment

Maoni yako