If you need it, we can provide: • USA 24 hours Passport service • Rush and emergency USA passport • Expedited Visa process for U.S. & foreign countries • Document Authentication •Document Legalization..For more information please contact us at: 703-286-7713

http://swahilivilla.blogspot.com/2014/01/mahojiano-na-faria-zam-kuhusu-msaada-wa.htmlKwa kuchangia chochote kile alichonacho kupitia Hilmy Disability Charity Organisation. Wasiliana na Mkurugezi wa Hilmy Disability Charity Organisation. Faria Zam. kwa UK Number ya Simu. 745-501-4372 Au Abou Shatry. U.S.A No' 301-728-3977

 http://www.dickysmallsauto.com/

DICK SMALLS AUTO MOTIVE WE CAN HANDLE ALL OF YOUR REPAIR AND SERVICE NEEDS INCLUDING CALL US NOW!(301) 931-3300. 10111B BACOCON DRIVE,BELTSVILLE,MD 20705


Monday, April 17, 2017

KENYA: MZOZO ODM IKIDAI MATIANG'I AMEWANYIMA VITUO VYA MCHUJO

Na LEONARD ONYANGO

KIZAAZAA kinatarajiwa baina ya chama cha ODM na waziri wa Elimu Fred Matiang'i kufuatia chama hicho kudai kuwa serikali inapanga kuzuilia chama hicho cha upinzani kufanyia kura za mchujo katika shule za umma.

Judith Pareno
Mwenyekiti wa Bodi ya Kitaifa ya Uchaguzi ya ODM (NEB) Judith Pareno akihutubia wanahabari Aprili 17, 2017. PICHA/ LEONARD ONYANGO

Mwenyekiti wa Bodi ya Kitaifa ya Uchaguzi ya ODM (NEB) Judith Pareno Jumatatu alisema kuwa Mkurugenzi wa Elimu wa Kaunti ya Kajiado tayari amepiga marufuku chama cha ODM kuendesha kura za mchujo katika shule za umma.

Kulingana na Bi Pareno, walimu wakuu wa baadhi ya shule katika maeneo ya Kitengela na Kajiado walifichua kwamba wamepokea agizo kutoka kwa Waziri Matiang'i kuzia kura za ODM kufanyikia katika shule zao.

"Tumepokea ripoti kuwa wakuu wa shule katika Kaunti ya Kajiado wamepata agizo kutoka kwa Waziri Matiang'i wasiruhusu chama cha ODM kufanya kura za mchujo shuleni.

Lakini napenda kuwahimiza wafuasi wa ODM kujitokeza katika shule hizo na kuteua viongozi wao wanaotaka kuwania viti kupitia tiketi ya ODM," akasema Bi Pareno.


Alisisitiza kuwa kura za mchujo za vyama vya kisiasa zinatambuliwa na katiba hivyo hazifai kutatizwa na serikali.

"Shule tunazotumia zimeorodheshwa katika gazeti rasmi la serikali kama vituo vya kupigia kura. Na sheria inaruhusu vyama vya kisiasa kufanyia kura za mchujo shuleni almradi wanafunzi wasiwe shuleni.

Hivyo shughuli ya kura za mchujo itaendelea kama ilivyopangwa na hatutatikiswa na Waziri Matiang'i," akasema Bi Pareno alipokuwa akihutubia wanahabari katika makao makuu ya ODM, Orange House.

No comments:

Post a Comment

Maoni yako