If you need it, we can provide: • USA 24 hours Passport service • Rush and emergency USA passport • Expedited Visa process for U.S. & foreign countries • Document Authentication •Document Legalization..For more information please contact us at: 703-286-7713

http://swahilivilla.blogspot.com/2014/01/mahojiano-na-faria-zam-kuhusu-msaada-wa.htmlKwa kuchangia chochote kile alichonacho kupitia Hilmy Disability Charity Organisation. Wasiliana na Mkurugezi wa Hilmy Disability Charity Organisation. Faria Zam. kwa UK Number ya Simu. 745-501-4372 Au Abou Shatry. U.S.A No' 301-728-3977

 http://www.dickysmallsauto.com/

DICK SMALLS AUTO MOTIVE WE CAN HANDLE ALL OF YOUR REPAIR AND SERVICE NEEDS INCLUDING CALL US NOW!(301) 931-3300. 10111B BACOCON DRIVE,BELTSVILLE,MD 20705

Tuesday, April 11, 2017

KENYA: NITAWANIA URAIS 2022, NAMWAMBA ATANGAZA

Na TITUS OTEBA

KIONGOZI wa chama cha Labour (LPK) Bw Ababu Namwamba Jumatatu alitangaza kuwa atakuwa debeni hapo 2022 kuwania urais.

Ababu
Kiongozi wa chama cha LPK Ababu Namwamba ahutubia wanahabari Aprili 4, 2017. PICHA/ LEONARD ONYANGO

Akihutubu katika kijiji cha Kimaet, kaunti ndogo ya Bumula baada ya kuwapokea wawaniaji watakaotumia tiketi za chama chake kugombea viti mbalimbali, Bw Namwamba alisema kwamba atamuunga mkono kiongozi wa chama cha ANC Bw Musalia Mudavadi au mwezake wa Ford Kenya Moses Wetang’ula iwapo watateuliwa kupeperusha bendera ya urais ya muungano wa Nasa.

“Kama si Mudavadi au Wetang’ula, Nasa isahau kura za jamii ya Waluhya. Hatuwezi kutumiwa na watu wengine kama ngazi ya kuingia ikulu. Jamii ya Waluhya ina roho safi, ina bidii na inaaminika na kwa maana hiyo, inafaa kupewa tiketi ya urais,” akasema.

Mbuge huyo wa Budalang’i alisisitiza kuwa ikiwa wawili hao watakosa kupewa nafasi kuongoza upinzani kumenyana na rais Kenyatta katika mbio za Ikulu, basi atawania urais ifikapo 2022.

Alisema kuwa taifa hili linahitaji rais kutoka jamii ya Waluhya ambaye atatatua changamoto zote zinazoikumba nchi kama ufisadi, ukosefu wa ajira, ugavi usio sawa wa mali ya umma na uongozi duni.


“Tunahitaji kurudisha mwenendo wa uwajibikaji, uaminifu, juhudi na ukweli katika siasa za Kenya. 

Mimi nina uwezo wa kutekeleza haya,” akasema.

Mbunge huyo alisisitiza kuwa yuko tayari kumuunga mkono Bw Wetang’ula na Bw Mudavadi kwa urais 2017 lakini wamwachie nafasi hiyo katika uchaguzi mkuu wa 2022 maanake ametimu kuongoza taifa hili.

Aliongeza kuwa hayuko tayari kumuunga mkono au kumpigia kura kiongozi wa chama cha ODM Raila Odinga iwapo Nasa itamteua kuwania urais.

Alimtaka Bw Mudavadi kuonyesha ukakamavu na kuchukua 'kilicho chake’ kwa sababu hawezi kuleta wazo la Nasa kisha asukumwe pembeni./

No comments:

Post a Comment

Maoni yako