If you need it, we can provide: • USA 24 hours Passport service • Rush and emergency USA passport • Expedited Visa process for U.S. & foreign countries • Document Authentication •Document Legalization..For more information please contact us at: 703-286-7713

http://swahilivilla.blogspot.com/2014/01/mahojiano-na-faria-zam-kuhusu-msaada-wa.htmlKwa kuchangia chochote kile alichonacho kupitia Hilmy Disability Charity Organisation. Wasiliana na Mkurugezi wa Hilmy Disability Charity Organisation. Faria Zam. kwa UK Number ya Simu. 745-501-4372 Au Abou Shatry. U.S.A No' 301-728-3977

 http://www.dickysmallsauto.com/

DICK SMALLS AUTO MOTIVE WE CAN HANDLE ALL OF YOUR REPAIR AND SERVICE NEEDS INCLUDING CALL US NOW!(301) 931-3300. 10111B BACOCON DRIVE,BELTSVILLE,MD 20705


Tuesday, April 11, 2017

Marekani yashambulia wanajeshi wa Syria na kudai inapambana na Daesh

Huku malalamiko ya walimwengu yakiwa bado yanaendelea dhidi ya shambulizi la makombora la Marekani katika maeneo ya wanajeshi wa Syria ambao wako mstari wa mbele kupambana na magaidi wakiwemo wa Daesh (ISIS), msemaji wa Ikulu ya Marekani White House jana alidai kuwa shabaha kuu ya Rais Donald Trump wa nchi hiyo na kupambana na mgaidi wa ISIS.

Sean Spicer amedai pia kuwa, shambulio la makombora la siku ya Ijumaa la Marekani limeungwa mkono na jamii ya kimataifa na kwamba bado kuna uwezekano Donald Trump akafanya mashambulizi mengine dhidi ya jeshi la Syria.

Madai hayo ya Ikulu ya Marekani ya kwamba eti inapambana na mgaidi wa Daesh nchini Syria yametolewa katika hali ambayo Ijumaa alfajiri, Donald Trump alifanya shambulizi la makumi ya makombora aina ya Tomahawk dhidi ya kituo cha jeshi la anga cha Shayrat nchini Syria na vijiji vya karibu na eneo hilo na kuua mamia ya watu wasio na hatia. Kambi hiyo ya kijeshi ina nafasi kubwa katika kupambana na magaidi wa ISIS na Jabhatun Nusra nchini Syria.

Kituo cha kijeshi cha al Shayrat nchini Syria

Marekani inadai imefanya mashambulizi hayo kujibu kile inachodai kuwa ni shambulio la silaha za kemikali la serikali ya Syria. 


Hata hivyo hakuna uchunguzi wowote uliofanyika hadi hivi sasa kuthibitisha iwapo shambulio hilo lilikuwa kweli ni la silaha za kemikali au la, na je ni serikali ya Syria au ni magenge ya kigaidi yaliyofanya shambulio hilo la Jumanne iliyopita.

Magaidi wanaendelea kupata pigo nchini Syria huku waungaji mkono wa magaidi hao hususan Marekani na utawala wa Kizayuni wa Israel na nchi kama Saudi Arabia, Qatar na Uturuki zikifanya kila njia kujaribu kuwarejeshea mori wa kufanya jinai zaidi magaidi hao./

No comments:

Post a Comment

Maoni yako