If you need it, we can provide: • USA 24 hours Passport service • Rush and emergency USA passport • Expedited Visa process for U.S. & foreign countries • Document Authentication •Document Legalization..For more information please contact us at: 703-286-7713

http://swahilivilla.blogspot.com/2014/01/mahojiano-na-faria-zam-kuhusu-msaada-wa.htmlKwa kuchangia chochote kile alichonacho kupitia Hilmy Disability Charity Organisation. Wasiliana na Mkurugezi wa Hilmy Disability Charity Organisation. Faria Zam. kwa UK Number ya Simu. 745-501-4372 Au Abou Shatry. U.S.A No' 301-728-3977

 http://www.dickysmallsauto.com/

DICK SMALLS AUTO MOTIVE WE CAN HANDLE ALL OF YOUR REPAIR AND SERVICE NEEDS INCLUDING CALL US NOW!(301) 931-3300. 10111B BACOCON DRIVE,BELTSVILLE,MD 20705


Tuesday, April 25, 2017

Mchakato wa kisiasa Burundi wazidi kugonga mwamba

Burundi inaelekea kuathiriwa tena na mgogoro wa kisiasa licha kufanyika juhudi za kikanda na kimataifa za kuupatia ufumbuzi mgogoro wa nchi hiyo.

Umoja wa Mataifa umeeleza kuwa, mgogoro wa kisiasa Burundi ambao ulianza kufuatia uamuzi wa Rais Pierre Nkurunziza wa nchi hiyo wa kusalia madarakani kwa muhula wa tatu mfululizo, umesababisha vifo vya watu elfu mbili, mamia ya wengine kutoweka na maelfu kuwa wakimbizi katika nchi jirani.

Wakimbizi wa Burundi waliokimbia machafuko nchini kwao


Benjamin Mkapa, Rais mstaafu wa Tanzania ambaye ni msuluhishi katika mgogoro wa kisiasa wa Burundi, ameshindwa kuandaa mazingira ya kufanyika mazungumzo kati ya serikali na wapinzani licha ya kupita miezi kadhaa hadi sasa, huku mashinikizo ya kimataifa kwa serikali ya Burundi yakisalia bila kuzaa matunda.

Leo Jumanne tarehe 25 Aprili ni siku ya kukumbuka kutumia mwaka wa pili tangu kuanza mgogoro wa kisiasa huko Burundi.

Chanzo: parstoday.com

No comments:

Post a Comment

Maoni yako