If you need it, we can provide: • USA 24 hours Passport service • Rush and emergency USA passport • Expedited Visa process for U.S. & foreign countries • Document Authentication •Document Legalization..For more information please contact us at: 703-286-7713

http://swahilivilla.blogspot.com/2014/01/mahojiano-na-faria-zam-kuhusu-msaada-wa.htmlKwa kuchangia chochote kile alichonacho kupitia Hilmy Disability Charity Organisation. Wasiliana na Mkurugezi wa Hilmy Disability Charity Organisation. Faria Zam. kwa UK Number ya Simu. 745-501-4372 Au Abou Shatry. U.S.A No' 301-728-3977

 http://www.dickysmallsauto.com/

DICK SMALLS AUTO MOTIVE WE CAN HANDLE ALL OF YOUR REPAIR AND SERVICE NEEDS INCLUDING CALL US NOW!(301) 931-3300. 10111B BACOCON DRIVE,BELTSVILLE,MD 20705

Thursday, April 6, 2017

Mfalme Salman wa Saudia ajifakharisha kwa kukutana na Theresa May wa Uingereza

Mfalme Salman bin Abdulaziz Al Saud wa Saudia amejifakharisha kwa kukutana na Waziri Mkuu wa Uingereza Theresa May ambaye nchi yake ndio mwasisi na muungaji mkono mkubwa wa utawala wa Aal-Saud na mashambulizi ya kila upande ya Saudia huko nchini Yemen.

Katika mkutano wao mjini Riyadh, Theresa May na Mfalme Salman bin Abdulaziz walijadili njia za kuimarisha ushirikiano wa nchi mbili hususan katika sekta ya kijeshi. 

May akiwa na ujumbe mkubwa amefanya safari nchini Saudia akiwa ametokea nchini Jordan ambapo alikutana na viongozi wa ngazi za juu wa Amman.

Mflalme wa Saudia na Waziri Mkuu wa Uingereza

Awali baada ya kuwasili Saudia Waziri Mkuu wa Uingereza alikutana na Muhammad bin Nayef, Mrithi wa kiti cha Ufalme wa taifa hilo ambapo walizungumzia ushirikiano wa nchi hizo. Itafahamika kuwa, Uingereza ni moja ya nchi muhimu zinazoiuzia silaha Saudia, ambazo zinatumika kushambulia raia madhlumu wa Yemen. 

Tangu Saudia ilipoanzisha hujuma hizo hadi leo yaani kuanzia mwezi Machi 2015, Uingereza ilitoa kibali cha kuiuzia silaha nchi hiyo chenye thamani ya zaidi ya pauni bilioni tatu. 

Mashambulizi hayo hadi sasa yamesababisha zaidi ya watu elfu 11 raia wa Yemen kuuawa na makumi ya maelfu ya wengine kujeruhiwa, huku zaidi ya watu milioni tatu wakiwa wakimbizi.

Hii ni katika hali ambayo wanaharakati mbalimbali Uingereza wamekuwa wakiendesha harakati ya kuitaka serikali ya nchi hiyo kukomesha siasa za kuiuzia silaha Saudia.
/

No comments:

Post a Comment

Maoni yako