If you need it, we can provide: • USA 24 hours Passport service • Rush and emergency USA passport • Expedited Visa process for U.S. & foreign countries • Document Authentication •Document Legalization..For more information please contact us at: 703-286-7713

http://swahilivilla.blogspot.com/2014/01/mahojiano-na-faria-zam-kuhusu-msaada-wa.htmlKwa kuchangia chochote kile alichonacho kupitia Hilmy Disability Charity Organisation. Wasiliana na Mkurugezi wa Hilmy Disability Charity Organisation. Faria Zam. kwa UK Number ya Simu. 745-501-4372 Au Abou Shatry. U.S.A No' 301-728-3977

 http://www.dickysmallsauto.com/

DICK SMALLS AUTO MOTIVE WE CAN HANDLE ALL OF YOUR REPAIR AND SERVICE NEEDS INCLUDING CALL US NOW!(301) 931-3300. 10111B BACOCON DRIVE,BELTSVILLE,MD 20705

Monday, April 10, 2017

NASA FARAGHANI KUGAWA NYADHIFA ZA SERIKALI

Na DANIEL NYASSY

VINARA wa muungano wa NASA, Jumapili walikutana faraghani mjini Mombasa kujadili jinsi ya kugawana mamlaka iwapo watashinda katika uchaguzi mkuu ujao na kuwataka wafuasi wao kuwa wavumilivu huku wakikamilisha mipango ya kutangaza mgombeaji wa urais.

National Super Alliance
Vigogo wa upinzani National Super Alliance (NASA) Musalia Mudavadi (kushoto), Kalonzo Musyoka, Raila Odinga, Moses Wetang'ula na Nick Salat wakiwa ukumbi wa Bomas Januari 11, 2017. Picha/JEFF ANGOTE

Kiongozi wa chama cha ODM Raila Odinga, Musalia Mudavadi wa chama cha Amani National Congress, Kalonzo Musyoka wa chama cha Wiper na Moses Wetang’ula wa chama cha Ford-Kenya walikutana baada ya kuhutubia mikutano ya hadhara katika maeneo ya Mombasa, Kilifi na Kwale.
Akiongea akiwa Kinango, Kwale, Bw Musyoka aliyeandamana na Bw Wetangula alisema: “Tutakutana kukubaliana na wakati ukifika tutatangaza mgombeaji wa urais.”

“Ninawaomba muwe na subira. Kila mmoja wetu anatosha kuwa rais. Hii ni timu inayolenga kuokoa nchi kutokana na uongozi mbaya,” alisema Bw Musyoka.

Bw Wetangula aliongeza: “Hatufichi chochote. Wakati ukifika tutawajulisha. Hata hivyo, tutakutana,” alisema Bw Wetangula.
Taifa Leo iligundua kwamba vinara hao walijadili jinsi ya kugawana nyadhifa za uwaziri na nyadhifa nyingine kuu serikalini, iwapo NASA itashinda katika uchaguzi mkuu ujao.

Tamasha

Nao Wabunge wa vyama vya ODM na Ford Kenya mnamo Jumamosi walisema Raila Odinga atakuwa mgombeaji urais wa NASA katika uchaguzi mkuu ujao.


Viongozi hao waliwaambia wafuasi wa muungano huo kwamba watulie kwa sababu tayari NASA ina mgombeaji wa urais.

Wabunge Jakoyo Midiwo (Gem), Gladys Wanga (Mwakilishi wa wanawake, Homa Bay ), Rose Nyamunga (Mwakilishi wa wanawake Kisumu ), Olago Aluoch (Kisumu Magharibi, Ford Kenya), James Nyikal (Seme), Nicholas Gumbo (Rarieda), Jared Kopiyo (Awendo, Ford Kenya), Shakeel Shabbir (Kisumu Mashariki ) na mwaniaji wa ugavana Hezron McObewa waliwataka viongozi wa Jubilee kukoma kuingilia masuala ya NASA.

Naibu Gavana wa Kisumu Ruth Odinga, alisema alikubali kuacha azma ya kugombea ugavana katika kaunti hiyo ili ndugu yake awe rais.

“Niliamua kuacha azma yangu ili kuhakikisha kwamba Raila atakuwa Rais wa nchi hii baada ya uchaguzi mkuu wa Agosti,” alisema.

Wabunge hao walikuwa wamehudhuria mazishi ya mama ya mbunge wa Muhoroni Onyango Koyoo, Bi Ludia Oyoo./

No comments:

Post a Comment

Maoni yako