If you need it, we can provide: • USA 24 hours Passport service • Rush and emergency USA passport • Expedited Visa process for U.S. & foreign countries • Document Authentication •Document Legalization..For more information please contact us at: 703-286-7713

http://swahilivilla.blogspot.com/2014/01/mahojiano-na-faria-zam-kuhusu-msaada-wa.htmlKwa kuchangia chochote kile alichonacho kupitia Hilmy Disability Charity Organisation. Wasiliana na Mkurugezi wa Hilmy Disability Charity Organisation. Faria Zam. kwa UK Number ya Simu. 745-501-4372 Au Abou Shatry. U.S.A No' 301-728-3977

 http://www.dickysmallsauto.com/

DICK SMALLS AUTO MOTIVE WE CAN HANDLE ALL OF YOUR REPAIR AND SERVICE NEEDS INCLUDING CALL US NOW!(301) 931-3300. 10111B BACOCON DRIVE,BELTSVILLE,MD 20705


Wednesday, April 26, 2017

Obama kuhutubia kuhusu mpango wake wa bima ya afya kwa ujira wa dola laki nne

Aliyekuwa rais wa Marekani Barack Obama atapokea donge nono la fedha kwa hotuba yake ya kwanza atakayotoa kwa malipo katika mkutano wa huduma ya afya utakaofanyika mwezi Septemba mwaka huu.

Kwa mujibu wa kanali ya televisheni ya PressTV, shirika la huduma za fedha la Cantor Fitzgerald, lenye makao yake mjini New York ambalo ndilo linaloandaa mkutano huo limemwomba rais huyo mstaafu wa Marekani atoe hotuba kuu ya mkutano na kuzungumzia mpango wake wa bima ya afya wa gharama nafuu maarufu kama Obamacare, ambao umepingwa na rais mpya wa nchi hiyo Donald Trump na ambaye ameahidi kuufuta.

Ripoti kuhusu kulipwa Obama kitita kikubwa cha fedha kwa ajili ya hotuba anayotazamiwa kutoa katika mkutano wa huduma za afya zimetolewa katika hali ambayo baada ya kimya cha zaidi ya miezi mitatu tangu Donald Trump aingie madarakani, siku ya Jumatatu iliyopita Barack Obama alivunja kimya chake kwa kutoa hotuba "bila ya malipo" katika Chuo Kikuu cha Chicago.

Obama alishiriki kwenye mezadura ya majadiliano iliyoshirikisha vijana lakini alikwepa kutoa maoni yoyote ya kisiasa au kumkosoa rais mpya wa Marekani.

Bill Clinton na mkewe Hillary Clinton


Obama hatokuwa rais kwanza mstaafu wa chama cha Democrat kujizolea donge nono la fedha kwa kutoa hotuba baada ya kuondoka Ikulu ya White House.

Imeripotiwa kuwa rais wa zamani wa nchi hiyo Bill Clinton pamoja na mkewe Hillary Clinton wamelipwa jumla ya dola milioni 153 kwa hotuba walizotoa kuanzia mwaka 2001 hadi 2015. Malipo ya hotuba hizo 729 ni wastani wa dola ya 210,795 kwa kila hotuba.../

Chanzo: parstoday.com

No comments:

Post a Comment

Maoni yako