If you need it, we can provide: • USA 24 hours Passport service • Rush and emergency USA passport • Expedited Visa process for U.S. & foreign countries • Document Authentication •Document Legalization..For more information please contact us at: 703-286-7713

http://swahilivilla.blogspot.com/2014/01/mahojiano-na-faria-zam-kuhusu-msaada-wa.htmlKwa kuchangia chochote kile alichonacho kupitia Hilmy Disability Charity Organisation. Wasiliana na Mkurugezi wa Hilmy Disability Charity Organisation. Faria Zam. kwa UK Number ya Simu. 745-501-4372 Au Abou Shatry. U.S.A No' 301-728-3977

 http://www.dickysmallsauto.com/

DICK SMALLS AUTO MOTIVE WE CAN HANDLE ALL OF YOUR REPAIR AND SERVICE NEEDS INCLUDING CALL US NOW!(301) 931-3300. 10111B BACOCON DRIVE,BELTSVILLE,MD 20705

Wednesday, April 5, 2017

Raia 3000 wa Sudan Kusini watorokea Uganda baada ya kushambuliwa na jeshi

Raia zaidi ya elfu 3 wa Sudan Kusini wameingia katika nchi jirani ya Uganda hii leo baada ya wanajeshi wa serikali SPLA kuvamia mji wa mpakani wa Pajok, na kuanza kufanya mauaji kiholela.

Mmoja wa watu walioponea chupuchupu katika mauaji hayo ambaye amejitambulisha kwa shirika la habari la Reuters kama Pasta Mondaa amesema kuwa, mji huo umebakia mahame baada ya aghalabu ya watu zaidi ya 52 elfu waliokuwa wakiishi hapo kukimbilia Uganda.

Ameongeza kuwa, akthari ya waliokuwa wakijaribu kukimbia waliuawa kwa kufyatuliwa risasi huku waliojisalimisha wakiuawa kwa kukatwa vichwa.

Duru za kiintelijiensia za Uganda zimeripoti kuwa, mashambulizi hayo dhidi ya wakazi wa mji wa Pakoj ulioko katika mpaka wa Uganda na Sudan Kusini yalianza jana Jumatatu na kwamba idadi kubwa ya watu wameuawa.

Askari wa jeshi la Sudan Kusini


Haya yanajiri katika hali ambayo, mwezi Februari mwaka huu, Umoja wa Mataifa ulisema wakimbizi 52,000 raia wa Sudan Kusini waliingia nchini Uganda mwezi uliopita pekee wa Januari, kutokana na kuendelea kushuhudiwa mauaji na machafuko katika nchi yao na kubainisha kuwa, watu wanauawa kwa umati na kutendewa jinai nyinginezo za kutisha katika eneo la Kajo-Keji. 

Aidha hivi karibuni takriban raia 35 elfu wa Sudan Kusini waliingia nchini Sudan kwa sababu ya ukame na kushadidi machafuko nchini mwao.

Waangalizi wa Umoja wa Mataifa wameikosoa serikali ya Sudan Kusini kwa mapigano yanayoendelea na kufichua kuwa, kati ya asilimia 97 ya mapato yanayotangazwa rasmi na serikali ya Juba kwamba yanatokana na mauzo ya mafuta, asilimia 50 ya mapato hayo inatumika kununua silaha.

Chanzo: parstoday.com

No comments:

Post a Comment

Maoni yako