If you need it, we can provide: • USA 24 hours Passport service • Rush and emergency USA passport • Expedited Visa process for U.S. & foreign countries • Document Authentication •Document Legalization..For more information please contact us at: 703-286-7713

http://swahilivilla.blogspot.com/2014/01/mahojiano-na-faria-zam-kuhusu-msaada-wa.htmlKwa kuchangia chochote kile alichonacho kupitia Hilmy Disability Charity Organisation. Wasiliana na Mkurugezi wa Hilmy Disability Charity Organisation. Faria Zam. kwa UK Number ya Simu. 745-501-4372 Au Abou Shatry. U.S.A No' 301-728-3977

 http://www.dickysmallsauto.com/

DICK SMALLS AUTO MOTIVE WE CAN HANDLE ALL OF YOUR REPAIR AND SERVICE NEEDS INCLUDING CALL US NOW!(301) 931-3300. 10111B BACOCON DRIVE,BELTSVILLE,MD 20705


Friday, April 28, 2017

Rais Magufuli aagiza kufutwa kazi kwa watumishi wa umma zaidi ya elfu 9

Na Victor Melkizedeck Abuso

Rais wa Tanzania John Magufuli ameagiza kufutwa kazi kwa zaidi ya wafanyikazi wa umma 9,900.

media
Rais wa Tanzania, John Pombe Magufuli, Dar es Salaam, Novemba 4, 2016.
Screenshot/Azama TV

Magufuli ametoa tangazo hili siku ya Ijumaa baada ya kupokea ripoti kuhusu uchunguzi wa wafanyikazi wa serikali waliotumia vyeti gushi i kupata kazi serikalini.

Aidha, ameitaka Wizara ya Fedha kutowalipa mshahara wafanyikazi hao waliobainika kuwa na vyeti hivyo baada ya uchunguzi kufanyika.

Kiongozi huyo ametaka majina ya wafanyikazi hao kuchapishwa katika magazeti ya nchini hiyo huku walioathirika wakitakiwa kuacha kazi mara moja.

“Watakaokataa kuondoka ikifika mwezi wa tano, watakumbana na mkono wa sheria na watafungwa jela miaka saba,” alisema Magufuli.


Katika hatua nyingine, Magufuli amesema kuwa hivi karibuni serikali yake itatangaza nafasi mpya 52,000 za kazi kwa raia wa nchi hiyo ya Afrika Mashariki.

Uamuzi huu wa rais Magufuli unakuja wakati huu dunia ikitarajiwa kuadhisha sikukuu ya Wafanyikazi tarehe 1 mwezi Mei, wiki ijayo.

Tanzania ni mojawapo ya nchi za bara la Afrika inayoendelea kukabiliwa na changamoto ya ajira haya kwa vijana.

Chanzo: sw.rfi.fr

No comments:

Post a Comment

Maoni yako