If you need it, we can provide: • USA 24 hours Passport service • Rush and emergency USA passport • Expedited Visa process for U.S. & foreign countries • Document Authentication •Document Legalization..For more information please contact us at: 703-286-7713

http://swahilivilla.blogspot.com/2014/01/mahojiano-na-faria-zam-kuhusu-msaada-wa.htmlKwa kuchangia chochote kile alichonacho kupitia Hilmy Disability Charity Organisation. Wasiliana na Mkurugezi wa Hilmy Disability Charity Organisation. Faria Zam. kwa UK Number ya Simu. 745-501-4372 Au Abou Shatry. U.S.A No' 301-728-3977

 http://www.dickysmallsauto.com/

DICK SMALLS AUTO MOTIVE WE CAN HANDLE ALL OF YOUR REPAIR AND SERVICE NEEDS INCLUDING CALL US NOW!(301) 931-3300. 10111B BACOCON DRIVE,BELTSVILLE,MD 20705


Wednesday, April 19, 2017

SIMUUNGI MKONO KENNETH, UHURU SASA ASEMA

Na WANDERI KAMAU

RAIS Uhuru Kenyatta Jumanne amekanusha ripoti kwamba anampendelea Bw Peter Kenneth kwenye kinyang’anyiro cha ugavana katika Kaunti ya Nairobi.

Rais Uhuru Kenyatta
Rais Uhuru Kenyatta akihutubu awali. Picha/PSCU

Kwenye taarifa kwa vyombo vya habari, Katibu Mkuu wa chama cha Jubilee Bw Raphael Tuju alisema kwamba rais amedumisha msimamo wake wa kutompendelea mwaniaji yeyote, huku shughuli za uteuzi zikizidi kukaribia.

“Rais hajamuunga mkono mwaniaji yeyote, kwani anaamini kwamba wakazi wa Nairobi watamchagua kiongozi wamtakaye kwa njia huru na yenye haki,” akasema Bw Tuju.

Hayo yanajiri kufuatia hisia kwamba huenda rais anampendelea Bw Kenneth dhidi ya Seneta Mike Sonko kufuatia matamshi yake Jumamosi katika eneo la Kirwara, kaunti ya Murang’a ambapo alimtaja Kenneth kama “shujaa.”

Rais Kenyatta na naibu wake William Ruto wameshikilia kwamba hawatamuunga mwaniaji yeyote kwenye shughuli za mchujo katika chama hicho, zilizopangiwa kufanyika Ijumaa katika kaunti 33 kote nchini.

“Tutatii uamuzi wa wananchi. Viongozi wengi wanaowania nyadhifa mbalimbali ni marafiki wetu, japo nyinyi (wananchi) ndio mtakuwa wenye usemi wa mwisho,” amenukuliwa Bw Kenyatta.


Kinyang’anyiro hicho kimezua ushindani mkali kati ya viongozi hao wawili, huku Bw Sonko akimtaja Kenneth kama “mgeni” asiyefahamu shida zinazowakabili wakazi wa Nairobi.

Kwa upande wake, Kenneth amesisitiza kwamba ana haki ya kuwania ugavana popote apendapo kama Mkenya.

Kumekuwa na hisia kwamba nia ya Bw Kenneth inasukumwa na mabwanyenye maarufu kutoka ukanda wa Mlima Kenya kwa lengo la “kulinda maslahi yao” jijini Nairobi.

Chanzo: swahilihub.com

No comments:

Post a Comment

Maoni yako