If you need it, we can provide: • USA 24 hours Passport service • Rush and emergency USA passport • Expedited Visa process for U.S. & foreign countries • Document Authentication •Document Legalization..For more information please contact us at: 703-286-7713

http://swahilivilla.blogspot.com/2014/01/mahojiano-na-faria-zam-kuhusu-msaada-wa.htmlKwa kuchangia chochote kile alichonacho kupitia Hilmy Disability Charity Organisation. Wasiliana na Mkurugezi wa Hilmy Disability Charity Organisation. Faria Zam. kwa UK Number ya Simu. 745-501-4372 Au Abou Shatry. U.S.A No' 301-728-3977

 http://www.dickysmallsauto.com/

DICK SMALLS AUTO MOTIVE WE CAN HANDLE ALL OF YOUR REPAIR AND SERVICE NEEDS INCLUDING CALL US NOW!(301) 931-3300. 10111B BACOCON DRIVE,BELTSVILLE,MD 20705

Sunday, April 9, 2017

Tahadhari kuhusu ukosefu wa usalama wa chakula katika eneo la Ziwa Chad

Shirika la Chakula na Kilimo la Umoja wa Mataifa (FAO) limetahadharisha kuwa kukosekana usalama wa chakula katika eneo la Ziwa Chad kunasababishwa na mashambulizi na hujuma za kundi la kigaidi la Boko Haram.

Graziano da Silva Mkurugenzi wa FAO ameitolea mwito jamii ya kimataifa izingatie pakubwa eneo la Ziwa Chad liloathiriwa na mashambulizi ya Boko Haram. Da Silva aliyasema hayo pambizoni mwa ziara yake katika nchi za eneo la Ziwa Chad hapo jana. 

Kuwepo wanamgambo wa kundi la Boko Haram na hali ya machafuko yanayosababishwa na kundi hilo, kumesababisha hasara kubwa kwa sekta ya kilimo na kuwafanya wakazi wa nchi nne za eneo la Ziwa Chad yaani Cameroon, Chad, Niger na Nigeria kushindwa kujidhaminia mahitaji yao ya chakuka.

Nchi zinazokabiliwa na ukame na ukosefu wa usalama wa chakula za Ziwa Chad

Shirika la Chakula na Kilimo la Umoja wa Mataifa (FAO) limeeleza kuwa watu milioni 69 wakazi wa eneo la Ziwa Chad hawana usalama wa chakula. 

Mkurugenzi wa FAO amekosoa kutotolewa fedha zilizoahidiwa kiasi cha dola milioni 672 katika mkutano wa mwezi Machi huko Norway na kueleza kuwa, wakazi wa eneo la Ziwa Chad watakabiliwa na hatari kubwa ya njaa kuliko ilivyokuwa huko nyuma iwapo halitazingatiwa suala la kutolewa bajeti na kukabiliana na ukame na ukosefu wa usalama kabla ya kuanza mwaka wa mavuno.

Chanzo: parstoday.com


/

No comments:

Post a Comment

Maoni yako