If you need it, we can provide: • USA 24 hours Passport service • Rush and emergency USA passport • Expedited Visa process for U.S. & foreign countries • Document Authentication •Document Legalization..For more information please contact us at: 703-286-7713

http://swahilivilla.blogspot.com/2014/01/mahojiano-na-faria-zam-kuhusu-msaada-wa.htmlKwa kuchangia chochote kile alichonacho kupitia Hilmy Disability Charity Organisation. Wasiliana na Mkurugezi wa Hilmy Disability Charity Organisation. Faria Zam. kwa UK Number ya Simu. 745-501-4372 Au Abou Shatry. U.S.A No' 301-728-3977

 http://www.dickysmallsauto.com/

DICK SMALLS AUTO MOTIVE WE CAN HANDLE ALL OF YOUR REPAIR AND SERVICE NEEDS INCLUDING CALL US NOW!(301) 931-3300. 10111B BACOCON DRIVE,BELTSVILLE,MD 20705

Tuesday, April 4, 2017

Trump achochea fitna Misri, aonana na el Sisi na kumwagia sifa

Rais Donald Trump wa Marekani ameonana na Rais Abdel Fattah el Sisi wa Misri na kummiminia sifa licha ya rais huyo kulalamikiwa vikali kwa kuvunja haki za binadamu katika nchi hiyo ya kaskazini mwa Afrika.

Trump amesema, ni fakhari kwake kuonana na Rais Abdul Fattah el Sisi wa Misri. Amesema, el Sisi ni mtu ambaye amekuwa karibu naye sana tangu walipoonana kwa mara ya kwanza. Amesema anakubaliana na el Sisi katika mambo mengi.

Donald Trump amenukuliwa akisema: "Napenda tu kukwambia Mheshimiwa Rais kwamba umepata rafiki mzuri wa kumtegemea huku Marekani, na rafiki huyo ni mimi.

Maandamano ya kumuunga rais wa zamani wa Misri na kumpinga Rais Abdul Fattah el Sisi nchini Marekani

Hata hivyo wapinzani wa Abdul Fattah el Sisi wanakihesabu kitendo hicho cha Rais wa Marekani cha kufumbia macho uvunjaji wa haki za binadamu na ukandamizaji anaoufanya ël Sisi dhidi ya wafuasi wa kundi la Ikhwanul Muslimin nchini Misri kuwa ni kueneza fitna na kuchochea ukandamizaji zaidi dhidi ya wananchi wa nchi hiyo. Raia wa Misri walioko nchini Marekani wamefanya maandamano wakimwita Jenerali Abdul Fattah el Sisi, mkuu wa zamani wa jeshi la Misri kuwa ni muuaji na mhalifu wa kivita.


Hii ni mara ya kwanza kwa Rais Abdul Fattah el Sisi kutembelea Marekani tangu alipoingia madarakani Donald Trump, kama ambavyo ni mara ya kwanza pia kwa el Sisi kutembelea Marekani tangu alipoingia madarakani nchini Misri mwaka 2014.

Ikumbukwe kuwa, kabla ya kuwa rais wa Misri, Jenerali Abdul Fattah el Sisi alikuwa mkuu wa jeshi la nchi hiyo na ndiye aliyeongoza mapinduzi ya kijeshi ya tarehe 4 Julai 2013 yaliyommg'oa madarakani rais wa kwanza kuchaguliwa kidemokrasia nchini Misri, Mohammad Morsi.
/

No comments:

Post a Comment

Maoni yako