If you need it, we can provide: • USA 24 hours Passport service • Rush and emergency USA passport • Expedited Visa process for U.S. & foreign countries • Document Authentication •Document Legalization..For more information please contact us at: 703-286-7713

http://swahilivilla.blogspot.com/2014/01/mahojiano-na-faria-zam-kuhusu-msaada-wa.htmlKwa kuchangia chochote kile alichonacho kupitia Hilmy Disability Charity Organisation. Wasiliana na Mkurugezi wa Hilmy Disability Charity Organisation. Faria Zam. kwa UK Number ya Simu. 745-501-4372 Au Abou Shatry. U.S.A No' 301-728-3977

 http://www.dickysmallsauto.com/

DICK SMALLS AUTO MOTIVE WE CAN HANDLE ALL OF YOUR REPAIR AND SERVICE NEEDS INCLUDING CALL US NOW!(301) 931-3300. 10111B BACOCON DRIVE,BELTSVILLE,MD 20705


Monday, April 24, 2017

UCHAGUZI WA MCHUJO JUBILEE WANG'OA NANGA

Na LAWRENCE ONGARO

UCHAGUZI wa mchujo wa viongozi wa Jubilee unastahili kuwa wa uwazi na wa haki bila visa vya vurugu miongoni mwa wapigaji kura, anasema Mbunge wa Gatundu Kaskazini.

Francis Kigo Njenga
Mbunge wa Gatundu Kaskazini, Francis Kigo Njenga. Picha/LAWRENCE ONGARO

Mbunge Francis Kigo Njenga, alisema bodi ya kusimamia uchaguzi katika chama cha Jubilee inastahili kuchukua hatua kali ya kufutilia mbali uchaguzi wa viongozi wanaozua vurugu kwa kuwanyima vyeti vya ushindi.

"Hatuwezi kukubali viongozi wachache kusababisha fujo kwa lengo la kupata nafasi ya uongozi kwa vile tunataka kuona haki ikitendeka kwa kila kiongozi ili kuwe na mwongozo mwema," alisema Njenga.

Alisema 2007 viongozi wachache walisababisha fujo na kujichukua kama walio juu ya sheria na bila hatua yoyote kuchukuliwa kulitokea fujo iliyoshuhudiwa baada ya uchaguzi huo.

"Wakati huu tungetaka vitengo husika kukaza buti na kuhakikisha hakuna mwanasiasa anasazwa kwa vyovyote,. Wakichukuliwa hatua bila shaka mambo yatakuwa katika mwelekeo ufaao," alisema Njenga.


Akiwahutubia waandishi wa habari eneo la Kamwangi wikendi, Gatundu Kaskazini, alisema uteuzi wa viongozi wa Jubilee ambao umeanza leo Jumatatu unastahili kuendeshwa kwa njia ya kuaminika na wote bila kubagua viongozi wachache.

Alisema iwapo wapigaji kura watagundua ya kwamba kiongozi wao ametendewa visivyo katika uteuzi huo bila shaka wengi wao watakosa kujitokeza kwa wingi wakati wa uchaguzi mkuu ujao wa Agosti 8, 2017.

"Tungetaka kuona ya kwamba kila kiongozi anachaguliwa kwa njia ya haki ili ifikapo uchaguzi mkuu wapigaji kura wajitokeze kwa wingi kumpigia rais Uhuru Kenyatta kura," alisema Njenga.

Alisema iwapo kiongozi atapoteza uchaguzi huo wa mchujo kwa njia isiyostahili bila shaka kuna uwezekano wa kuwaelekeza wafuasi wake katika mkondo mwingine tofauti na hilo linaweza kupunguza kura za rais katika chama cha Jubilee.

No comments:

Post a Comment

Maoni yako