If you need it, we can provide: • USA 24 hours Passport service • Rush and emergency USA passport • Expedited Visa process for U.S. & foreign countries • Document Authentication •Document Legalization..For more information please contact us at: 703-286-7713

http://swahilivilla.blogspot.com/2014/01/mahojiano-na-faria-zam-kuhusu-msaada-wa.htmlKwa kuchangia chochote kile alichonacho kupitia Hilmy Disability Charity Organisation. Wasiliana na Mkurugezi wa Hilmy Disability Charity Organisation. Faria Zam. kwa UK Number ya Simu. 745-501-4372 Au Abou Shatry. U.S.A No' 301-728-3977

 http://www.dickysmallsauto.com/

DICK SMALLS AUTO MOTIVE WE CAN HANDLE ALL OF YOUR REPAIR AND SERVICE NEEDS INCLUDING CALL US NOW!(301) 931-3300. 10111B BACOCON DRIVE,BELTSVILLE,MD 20705

Sunday, April 2, 2017

Uhusiano wa kifedha wa mshauri wa zamani wa usalama wa taifa wa Marekani na Russia wafichuka

Ikulu ya Marekani White House imetoa nyaraka mpya zinazoonesha kuwa mshauri wa zamani wa usalama wa taifa wa nchi hiyo alikuwa anapokea fedha kutoka Russia.

Kwa mujibu wa Press TV, nyaraka mpya zilizotolewa tarehe 1 Aprili 2017 na Ikulu ya Marekani (White House) zinaonesha kuwa Michael T. Flynn, mshauri wa zamani wa usalama wa taifa wa Rais Donald Trump wa Marekani alikiri katika orodha yake iliyohusiana na vyanzo vilivyokuwa vinavyomuingizia fedha kuwa ni pamoja na televisheni ya Russia Today na shirika la usafiri wa anga la Russia lijulikanalo kwa jina la Volga-Dnepr Airlines.

Fomu ya maswali kuhusiana na vyanzo vya fedha alivyokuwa akivitumia mshauri huyo wa zamani wa usalama wa taifa wa Marekani iliorodhesha fedha alizokuwa akizipata kutokana na hotuba zake.

Rais Donald Trump wa Marekani na mshauri wake wa usalama wa taifa Michael Flynn ambaye amepatikana na kashfa ya kupokea fedha kutoka Russia na kuwa na mawasiliano na balozi wa nchi hiyo mjini Washington


Yaliyomo kwenye fomu hiyo yalisambazwa mwezi wa Januari mwaka huu yaani siku chache kabla ya kujiuzulu kwake baada ya kukumbwa na kashfa na kuwa na uhusiano na Sergey Ksiliyak, balozi wa Russia mjini Washington, Sergei Kislyak.

Katika siku za hivi karibuni, maafisa wa White House walimshauri mshauri huyo wa zamani wa usalama wa taifa wa Marekani ataje kila shirika moja moja lililokuwa linamlipa fedha.

Michael Flynn alilazimika kujiuzulu baada ya kubainika kwamba alikuwa na mawasiliano na balozi wa Russia mjini Washington.
/

No comments:

Post a Comment

Maoni yako