If you need it, we can provide: • USA 24 hours Passport service • Rush and emergency USA passport • Expedited Visa process for U.S. & foreign countries • Document Authentication •Document Legalization..For more information please contact us at: 703-286-7713

http://swahilivilla.blogspot.com/2014/01/mahojiano-na-faria-zam-kuhusu-msaada-wa.htmlKwa kuchangia chochote kile alichonacho kupitia Hilmy Disability Charity Organisation. Wasiliana na Mkurugezi wa Hilmy Disability Charity Organisation. Faria Zam. kwa UK Number ya Simu. 745-501-4372 Au Abou Shatry. U.S.A No' 301-728-3977

 http://www.dickysmallsauto.com/

DICK SMALLS AUTO MOTIVE WE CAN HANDLE ALL OF YOUR REPAIR AND SERVICE NEEDS INCLUDING CALL US NOW!(301) 931-3300. 10111B BACOCON DRIVE,BELTSVILLE,MD 20705

Saturday, April 8, 2017

UNICEF: Watoto 269 walio chini ya miaka mitano hufariki dunia kila siku Tanzania

Shirika la Kuhudumia Watoto la Umoja wa Mataifa (UNICEF) limesema kuwa, jumla ya watoto 269 wenye umri wa chini ya miaka mitano hufariki dunia kila siku nchini Tanzania.

Hayo yalisemwa leo na mwakilishi wa (UNICEF) nchini Tanzania Maniza Zaman kwenye mkutano wa Jukwaa la Wahariri (TEF) huko mjini Moshi. 

Aidha ameongeza kuwa, jumla ya wajawazito 556 hufariki dunia pia kutokana na matatizo mbalimbali ya uzazi ndani ya taifa hilo, suala linalotishia maisha ya akina mama.

Zaman amesema kuwa, kwa mujibu wa utafiti walioufanya kuhusiana na masuala ya elimu kwa watoto, ni asilimia 39 tu ya watoto wa kike na kiume ndio wanaohitimu elimu ya sekondari nchini humo kila mwaka licha ya juhudi kubwa zinazofanywa na serikali katika uwanja huo. 

Maniza Zaman ameitaka serikali kushirikiana na asasi mbalimbali za kujitegemea kuwekeza katika masuala ya watoto hususan katika sekta za elimu na huduma bora za afya ili kuepusha vifo vya watoto wadogo./

No comments:

Post a Comment

Maoni yako