If you need it, we can provide: • USA 24 hours Passport service • Rush and emergency USA passport • Expedited Visa process for U.S. & foreign countries • Document Authentication •Document Legalization..For more information please contact us at: 703-286-7713

http://swahilivilla.blogspot.com/2014/01/mahojiano-na-faria-zam-kuhusu-msaada-wa.htmlKwa kuchangia chochote kile alichonacho kupitia Hilmy Disability Charity Organisation. Wasiliana na Mkurugezi wa Hilmy Disability Charity Organisation. Faria Zam. kwa UK Number ya Simu. 745-501-4372 Au Abou Shatry. U.S.A No' 301-728-3977

 http://www.dickysmallsauto.com/

DICK SMALLS AUTO MOTIVE WE CAN HANDLE ALL OF YOUR REPAIR AND SERVICE NEEDS INCLUDING CALL US NOW!(301) 931-3300. 10111B BACOCON DRIVE,BELTSVILLE,MD 20705


Tuesday, April 18, 2017

Waislamu Nigeria waandamana kwa amani, polisi wawakandamiza

Vikosi vya usalama vya Nigeria kwa mara nyingine tena vimekandamiza maandamano ya amani ya Waislamu wa nchi hiyo.

Shirika la habari la FARS limeripoti habari hiyo na kuongeza kuwa, Waislamu hao wameandamana kwa njia ya amani katika mji mkuu wa Nigeria Abuja, ili kuishinikiza serikali kutekeleza amri ya mahakama ya kumwachilia huru Sheikh Ibrahim Zakzaky, mkuu wa Harakati ya Kiislamu ya Nigeria, hata hivyo polisi wa nchi hiyo wametumia mabomu ya kutoa machozi na maji ya sumu kuwatawanya mamia ya Waislamu hao.

Sheikh Ibrahim Zakzaky, Mkuu wa Harakati ya Kiislamu ya Nigeria

Wengi wa Waislamu hao walikuwa ni wanawake na waliitisha maandamano hayo jana ili kuishinikiza serikali imwachilie huru Sheikh Zakzaky ambaye anaendelea kushikiliwa na serikali licha ya Mahakama Kuu ya Nigeria kutoa amri ya kuachiliwa huru.

Sheikh Zakzaky alitekwa nyara na jeshi la Nigeria mwezi Disemba 2015 baada ya kupigwa risasi na kujeruhiwa vibaya na jeshi hilo, na tangu wakati huo hadi hivi sasa serikali ya nchi hiyo inayoongozwa na Rais Muhammadu Buhari inaendelea kumshikilia kinyume cha sheria.

Chanzo: parstoday.com

No comments:

Post a Comment

Maoni yako