If you need it, we can provide: • USA 24 hours Passport service • Rush and emergency USA passport • Expedited Visa process for U.S. & foreign countries • Document Authentication •Document Legalization..For more information please contact us at: 703-286-7713

http://swahilivilla.blogspot.com/2014/01/mahojiano-na-faria-zam-kuhusu-msaada-wa.htmlKwa kuchangia chochote kile alichonacho kupitia Hilmy Disability Charity Organisation. Wasiliana na Mkurugezi wa Hilmy Disability Charity Organisation. Faria Zam. kwa UK Number ya Simu. 745-501-4372 Au Abou Shatry. U.S.A No' 301-728-3977

 http://www.dickysmallsauto.com/

DICK SMALLS AUTO MOTIVE WE CAN HANDLE ALL OF YOUR REPAIR AND SERVICE NEEDS INCLUDING CALL US NOW!(301) 931-3300. 10111B BACOCON DRIVE,BELTSVILLE,MD 20705

Friday, April 21, 2017

Waziri Mkuu wa Korea Kusini, atoa amri kulitaka jeshi la nchi hiyo lijiweke tayari kukabiliana na Pyongyang

Waziri Mkuu wa Korea Kusini anayekaimu nafasi ya rais, amelitaka jeshi na vikosi vya nchi hiyo kujiweka tayari kutokana na kile alichokisema kuwa ni kushadidi kwa harakati za kijeshi za Pyongyang.

Hwang Kyo-ahn ameyasema hayo Alkhamis ya leo katika kikao cha Baraza la Mawaziri la Korea Kusini kufuatia kuenea kwa habari zinazohusiana na uwezekano wa Korea Kaskazini kufanya jaribio la sita la silaha ya nyuklia hivi karibuni. 

Kufuatia hali hiyo Hwang Kyo-ahn ametoa amri kwa jeshi la nchi yake kujiweka tayari kwa ajili ya kukabiliana na hatua yoyote ya kijeshi na harakati za Korea Kaskazini.

Jeshi la Korea Kusini

Kadhalika Waziri Mkuu wa Korea Kusini amelitaka jeshi la nchi hiyo kufuatilia kwa karibu mabadiliko na harakati zote za Pyongyang. 

Mgogoro katika eneo la Peninsula ya Korea ulishadidi baada ya Rais Donald Trum wa Marekani na makamu wake wa rais, Mike Pence kutoa matamshi ya vitisho kuilenga Pyongyang, vitisho ambavyo vilienda sambamba na kutumwa kwa meli tatu za kijeshi zinazobeba ndege za kivita karibu na pwani ya Korea Kaskazini.


Hwang Kyo-ahn, Waziri Mkuu wa Korea Kusini

Hatua hiyo ya Marekani ilitajwa na Korea Kaskazini kuwa, ya kichokozi na inayohatarisha usalama na amani ya peninsula hiyo. Mbali na hayo ni kwamba Korea Kaskazini imesisitiza mara kadhaa kwamba, madamu Marekani na waitifaki wake zitaendelea kutishia usalama wake, basi nayo itazidi kuimarisha uwezo wake wa kijeshi kukabiliana na chokochoko za adui.

Chanzo: parstoday.com

No comments:

Post a Comment

Maoni yako