If you need it, we can provide: • USA 24 hours Passport service • Rush and emergency USA passport • Expedited Visa process for U.S. & foreign countries • Document Authentication •Document Legalization..For more information please contact us at: 703-286-7713

http://swahilivilla.blogspot.com/2014/01/mahojiano-na-faria-zam-kuhusu-msaada-wa.htmlKwa kuchangia chochote kile alichonacho kupitia Hilmy Disability Charity Organisation. Wasiliana na Mkurugezi wa Hilmy Disability Charity Organisation. Faria Zam. kwa UK Number ya Simu. 745-501-4372 Au Abou Shatry. U.S.A No' 301-728-3977

 http://www.dickysmallsauto.com/

DICK SMALLS AUTO MOTIVE WE CAN HANDLE ALL OF YOUR REPAIR AND SERVICE NEEDS INCLUDING CALL US NOW!(301) 931-3300. 10111B BACOCON DRIVE,BELTSVILLE,MD 20705


Tuesday, April 18, 2017

Waziri mkuu wa Uingereza Theresa May aitisha uchaguzi mkuu mwezi Juni

Na Emmanuel Richard Makundi

Waziri mkuu wa Uingereza Theresa May ametangaza mpango wa kuitisha uchaguzi mkuu June 8 mwaka huu.

media
Waziri mkuu wa Uingereza Theresa May. 18 April 2017.
REUTERS/Toby Melville

Waziri mkuu May amesema kuwa Uingereza inahitaji uthabiti na njia safi pamoja na utawala imara baada ya kufanyika kwa kura ya maoni kujitoa kwenye umoja wa Ulaya.

Akielezea ni kwanini ameamua kuitisha kura hiyo, May amesema nchi inakuja pamoja lakini wabunge wa Westminster hawako pamoja.

Ameongeza kuwa Jumatano ya wiki hii kutakuwa na kura ya mapendekezo kuhusu uchaguzi huu, na atahitaji bunge kuidhinisha mpango wake wa kufanya uchaguzi mkuu kabla ya 2020.

Akifafanua ni vipi ameamua kubadili mtazamo na kuitisha uchaguzi wa mapema, waziri mkuu May amesema "nimehitmisha kuwa njia pekee ya kuwa na umakini na usalama kwa miaka ijayo ni kwa kufanya uchaguzi."


May wamevishutumu vyama vingine vya upinzani kwa kufanya mchezo wa kitoto akisema mchezo huo utakwamisha mchakato wa nchi yao kujitoa umoja wa Ulaya na utatatiza uimara wa taifa lake.

"Kwa hivyo tunahitaji uchaguzi mkuu mpya na tunauhitaji sasa. Tuna wakati huu mmoja pekee wa kufanya hili." alisema May.

Chanzo: sw.rfi.fr

No comments:

Post a Comment

Maoni yako