If you need it, we can provide: • USA 24 hours Passport service • Rush and emergency USA passport • Expedited Visa process for U.S. & foreign countries • Document Authentication •Document Legalization..For more information please contact us at: 703-286-7713

http://swahilivilla.blogspot.com/2014/01/mahojiano-na-faria-zam-kuhusu-msaada-wa.htmlKwa kuchangia chochote kile alichonacho kupitia Hilmy Disability Charity Organisation. Wasiliana na Mkurugezi wa Hilmy Disability Charity Organisation. Faria Zam. kwa UK Number ya Simu. 745-501-4372 Au Abou Shatry. U.S.A No' 301-728-3977

 http://www.dickysmallsauto.com/

DICK SMALLS AUTO MOTIVE WE CAN HANDLE ALL OF YOUR REPAIR AND SERVICE NEEDS INCLUDING CALL US NOW!(301) 931-3300. 10111B BACOCON DRIVE,BELTSVILLE,MD 20705


Monday, May 8, 2017

BEI GHALI YASUKUMA WAKENYA KUNUNUA SUKARI TANZANIA

Na ELISHA OTIENO

Katika kaunti ya Migori, wafanyabiashara wamekuwa wakisafiri hadi nchi hiyo jirani kununua bidhaa hiyo inayouzwa kwa bei nafuu.

Sukari hatari yadaiwa kuuziwa raia nchini
Mwanamume akiwa na sukari akilalamikia serikali kuhusu ugumu wa maisha awali. Picha/PHOEBE OKAL

Kilo moja ya sukari inauzwa kwa kati ya Sh110 na Sh120 lakini hapa Kenya inauzwa kwa Sh200 na kuwafanya wafanyabiashara kupata faida kubwa.

Hata hivyo, baadhi ya wateja wanalalamika kuwa sukari hiyo ni ya kiwango duni.

“Unaweka vijiko vinne vya sukari hiyo katika kikombe cha chai ili upate ladha yake. Sio nzuri japo ni ya bei nafuu,” alilalamika Bi Eunice Odol mwenye umri wa miaka 34.

Sukari hiyo inatoka kiwanda cha sukari cha Kilombero kilichoko Mwanza, Tanzania. Kulingana na uchunguzi wa Taifa Leo, sukari hiyo inauzwa kwa pakiti zilizo na nembo ya kiwanda hicho.

Baadhi ya maduka makubwa katika kaunti ya Migori pia yanauza sukari kutoka Tanzania huku bei za bidhaa muhimu zikiendelea kupanda.

Bei ya unga wa mahindi nchini ilipanda hadi Sh200 kutoka Sh170. Wateja waliuziwa pakiti moja ya kilo mbili katika baadhi ya maduka makubwa kutokana na uhaba wa bidhaa hiyo nchini.


Bei imekuwa ikipanda licha ya viongozi kulilia serikali kuchukua hatua kuokoa Wakenya wanaolemewa na kupanda kwa gharama ya maisha.

Akiongea katika sherehe za Siku ya Wafanyakazi ulimwenguni katika bustani ya Uhuru Park wiki jana, Rais Uhuru Kenyatta alisema kwamba serikali inachukua hatua za kupunguza bei ya vyakula.

Afisa wa kiwanda cha sukari cha Sony ambaye aliomba tusitaje jina lake kwa sababu haruhusiwi kuzungumza na wanahabari alilalamika kwamba baadhi ya sukari inayouzwa nchini kinyume cha sheria inapakiwa katika pakiti zilizo na jina la kampuni yao.

Ulaghai

“Wateja wanapasa kuwa waangalifu sana ili wasitapeliwa na walaghai wanaofanya biashara ya sukari ambao wanaingia sukari ya kiwango cha chini na kuipakia kwenye karatasi zilizo na nebo ya kiwanda chetu,” alisema.

Bidhaa nyingine zinazonunuliwa kutoka Tanzania ni mchele, bidhaa za urembo na dawa ya meno.
Idara ya taifa ya sukari Kenya ililaumu wafanyabiashara wenye tamaa kwa kuficha bidhaa hiyo na kusababisha uhaba uliopo.

Mkuu wa idara hiyo Solomon Odera alisema bei ya Sh380 kwa pakiti ya kilo mbili ya sukari inasababishwa na hatua ya wafanyabiashara ya kuficha bidhaa hiyo.

Alisema idara hiyo imeagiza tani 100,000 za sukari kutoka soko la pamoja la mataifa ya Mashariki na Kusini mwa Afrika (Comesa) ili kulazimisha viwanda vya sukari kuachilia wanayoficha.

Chanzo: swahilihub.com

No comments:

Post a Comment

Maoni yako