If you need it, we can provide: • USA 24 hours Passport service • Rush and emergency USA passport • Expedited Visa process for U.S. & foreign countries • Document Authentication •Document Legalization..For more information please contact us at: 703-286-7713

http://swahilivilla.blogspot.com/2014/01/mahojiano-na-faria-zam-kuhusu-msaada-wa.htmlKwa kuchangia chochote kile alichonacho kupitia Hilmy Disability Charity Organisation. Wasiliana na Mkurugezi wa Hilmy Disability Charity Organisation. Faria Zam. kwa UK Number ya Simu. 745-501-4372 Au Abou Shatry. U.S.A No' 301-728-3977

 http://www.dickysmallsauto.com/

DICK SMALLS AUTO MOTIVE WE CAN HANDLE ALL OF YOUR REPAIR AND SERVICE NEEDS INCLUDING CALL US NOW!(301) 931-3300. 10111B BACOCON DRIVE,BELTSVILLE,MD 20705


Saturday, May 13, 2017

Boko Haram yatishia kuushambulia mji mkuu wa Nigeria Abuja

Kundi la kigaidi la Boko Haram limetishia kwamba, litafanya mashambulio dhidi ya mji mkuu wa Nigeria Abuja.

Shirika la Habari la Sahara Reporters limetoa mkanda wa video unaomuonyesha mtu mmoja anayedai kuwa mmoja wa wanachama wa Boko Haram ambaye anasisitiza katika mkanda huo wa video kwamba, mashambulio mengi ya mabomu ya kundi hilo yapo njiani na miongoni mwa maeneo yatakayolengwa ni mji mkuu Abuja.

Mkanda huo wa video wa vitisho unasambazwa katika hali ambayo mwanzoni mwa mwezi huu vyombo vya usalama vya Nigeria vilidai kwamba, Abubakar Shekau, kiongozi wa kundi la kigaidi la Boklo Haram alijeruhiwa katika shambulio la ndege za kijeshi katika kijiji cha Balla kwenye jimbo la Borno lililoko kaskazini mashariki mwa nchi hiyo ya magharibi mwa Afrika.

Wanachama wa Boko Haram

Kundi la Boko Haram lilianzisha mashambulizi dhidi ya maeneo ya umma na taasisi za serikali huko kaskazkini mwa Nigeria mwaka 2009 na baadaye mwaka 2015 likapanua mashambulizi hayo hadi katika nchi za Chad, Cameroon na Niger.


Zaidi ya watu elfu 20 wameuwa hadi sasa katika mashambulizi hayo na wengine zaidi ya milioni mbili wamelazimika kuwa wakimbizi.

Serikali ya Nigeria inayoongozwa na Rais Muhammad Buhari imeendelea kukosolewa vikali kutokana na kile kinachoelezwa kuwa, kushindwa serikali yake kukabiliana na kundi hilo ambalo limetenda jinai nyingi.

Chanzo: parstoday.com

No comments:

Post a Comment

Maoni yako