If you need it, we can provide: • USA 24 hours Passport service • Rush and emergency USA passport • Expedited Visa process for U.S. & foreign countries • Document Authentication •Document Legalization..For more information please contact us at: 703-286-7713

http://swahilivilla.blogspot.com/2014/01/mahojiano-na-faria-zam-kuhusu-msaada-wa.htmlKwa kuchangia chochote kile alichonacho kupitia Hilmy Disability Charity Organisation. Wasiliana na Mkurugezi wa Hilmy Disability Charity Organisation. Faria Zam. kwa UK Number ya Simu. 745-501-4372 Au Abou Shatry. U.S.A No' 301-728-3977

 http://www.dickysmallsauto.com/

DICK SMALLS AUTO MOTIVE WE CAN HANDLE ALL OF YOUR REPAIR AND SERVICE NEEDS INCLUDING CALL US NOW!(301) 931-3300. 10111B BACOCON DRIVE,BELTSVILLE,MD 20705

Monday, May 29, 2017

Israel yafaidika na mkataba wa silaha wa Saudia, Marekani

Gazeti moja la Kizayuni, limefichua kuwa, katika mkataba wa mabilioni ya dola wa ununuzi silaha baina ya Marekani na Saudia, mashirika ya Israel yatapata faida kubwa sana.

Televisheni ya Al Alam imenukulu duru za Kizayuni zikisema, mashirika mengi ya uundaji silaha ya Israel yana mikataba na mashirika ya utengenezaji silaha ya Marekani ambayo yanaiuzia Saudia silaha.

Awamu ya kwanza ya Mkataba wa ununuzi silaha uliotowa saini hivi karibuni baina ya Saudia na Marekani wakati Rais Donald Trump alipokuwa mjini Riyadh, itagharimu dola bilioni 110. Mkataba huo unatzamiwa kufika dola biliini 350 katika kipindi cha miaka 10 ijayo.

Taarifa zinasema mkataba huo utapeleeka mashirika ya kutengeneza silaha ya Israel kuweza kupata faida kubwa na yamedhaminiwa faida hiyo kwa muda wa miaka 10.

Ndege ya kivita ya Saudia

Duru za Kizayuni zinadokeza kuwa: "Mashirika ya kuunda zana za kijeshi ya Marekani kama vile Lockheed Martin ambayo yana jukumu la kuiuzia Saudia silaha na mifumo ya kivita yametakiwa kushirikiana na Shirika la Kuunda Silaha la Israel la Rafael."


Afisa wa Wizara ya Vita ya Israel ambaye hakutaka jina lake litajwe naye pia amesema mkataba mkubwa wa silaha baina ya Marekani na Saudia ni jambo ambalo litaimarisha uwezo wa mashirika ya Israel.

Wakati wa kutiwa saini mkataba huo wa silaha, Rais Donald Trump alitangaza wazi kuwa lengo lake ni kubuni ajira kwa ajili ya Wamarekani huku akijigamba kuwa amefanikiwa kuchukua mabilioni ya dola za fedha za Saudia na kuzipeleka Marekani.

Chanzo: parstoday.com

No comments:

Post a Comment

Maoni yako