If you need it, we can provide: • USA 24 hours Passport service • Rush and emergency USA passport • Expedited Visa process for U.S. & foreign countries • Document Authentication •Document Legalization..For more information please contact us at: 703-286-7713

http://swahilivilla.blogspot.com/2014/01/mahojiano-na-faria-zam-kuhusu-msaada-wa.htmlKwa kuchangia chochote kile alichonacho kupitia Hilmy Disability Charity Organisation. Wasiliana na Mkurugezi wa Hilmy Disability Charity Organisation. Faria Zam. kwa UK Number ya Simu. 745-501-4372 Au Abou Shatry. U.S.A No' 301-728-3977

 http://www.dickysmallsauto.com/

DICK SMALLS AUTO MOTIVE WE CAN HANDLE ALL OF YOUR REPAIR AND SERVICE NEEDS INCLUDING CALL US NOW!(301) 931-3300. 10111B BACOCON DRIVE,BELTSVILLE,MD 20705


Monday, May 1, 2017

JAGUAR ALILSAFIRISHA WAPIGA KURA KUTOKA NJE KUNISHINDA - KAMANDA

Na WANDERI KAMAU

MBUNGE wa Starehe Maina Kamanda amedai kwamba baadhi ya maafisa wakuu katika Chama cha Jubilee (JP) wanapanga njama za kumnyang’anya ushindi wa tiketi ya chama hicho.

Maina Kamanda
Mbunge wa Starehe Maina Kamanda akiongea katika kikao cha awali na wanahabari Nairobi. Picha/ANTHONY OMUYA

Bw Kamanda alisema jana kwamba uhesabu mpya wa kura umeonyesha kuwa aliibuka mshindi kwa kupata kura 11,337 dhidi ya kura 10, 374 ambazo alikuwa ametangazwa kupata awali kwenye shughuli za mchujo.

Kwenye kikao na wanahabari katika makao makuu ya chama hicho, jijini Nairobi Jumatatu, mbunge huyo alimlaumu mpinzani wake mkuu, mwanamuziki Charles Njagua “Jaguar” kwa kuwasafirisha baadhi ya wapigakura kutoka nje ya eneobunge hilo, aliodai hawajasajiliwa huko. Bw Njagua alitajwa kupata kura 8, 391 ila amekuwa akisisitiza kwamba ndiye aliibuka mshindi.

Bw Kamanda alimtaja afisa mmoja kama balozi wa zamani, ambaye amekuwa akiendesha njama za kichinichini kuhakikisha kuwa mwanamuziki huyo amepata tiketi hiyo.

“Mmoja wa maafisa hao ni balozi wa zamani ambaye aliingizwa kichinichini na Katibu Mkuu Raphael Tuju kusimamia masuala ya chama. Tuna ushahidi wa wazi kwamba anashirikiana kisiri na mshindani wangu,” akasema Bw Kamanda, aliyeonekana mwenye ghadhabu.


Alidai kwamba balozi huyo wa zamani ni miongoni mwa maafisa wengine wengi ambao wamekuwa wakiingizwa kisiri kusimamia shughuli hizo.

Alisema kuwa ingawa ataendelea kungoja maamuzi ya mwisho ya kitengo cha malalamishi chamani, hatakubali uamuzi wowote utakaomnyang’anya tiketi hiyo, kwani ni wazi kwamba aliibuka mshindi kihalali.

“Ni lazima nipewe tiketi yangu. La sivyo, chama hiki huenda kikapoteza umaarufu wake jijino kwa ukosefu wa uwazi,” akasema Bw Kamanda, aliyeandamana na wafuasi wake.

Kauli ya Bw Kamanda inajiri siku moja baada ya mwanamuziki huyo kudondokwa na machozi hadharani, akidai kwamba alinyang’anywa ushindi wake kiwazi.

Matokeo ya mchujo huo yalitolewa mnamo Jumanne iliyopita katika Shule ya Upili ya Jamhuri, ambapo wafuasi wa Bw Njagua walidai kwamba matokeo hayo “yalighushiwa” muda mfupi baada ya Bw Kamanda kufika katika ukumbi wa kuhesabia kura.

Chama kinatarajiwa kutoa uamuzi wake kuhusu mzozo huo Jumanne.

Chanzo: swahilihub.com

No comments:

Post a Comment

Maoni yako