If you need it, we can provide: • USA 24 hours Passport service • Rush and emergency USA passport • Expedited Visa process for U.S. & foreign countries • Document Authentication •Document Legalization..For more information please contact us at: 703-286-7713

http://swahilivilla.blogspot.com/2014/01/mahojiano-na-faria-zam-kuhusu-msaada-wa.htmlKwa kuchangia chochote kile alichonacho kupitia Hilmy Disability Charity Organisation. Wasiliana na Mkurugezi wa Hilmy Disability Charity Organisation. Faria Zam. kwa UK Number ya Simu. 745-501-4372 Au Abou Shatry. U.S.A No' 301-728-3977

 http://www.dickysmallsauto.com/

DICK SMALLS AUTO MOTIVE WE CAN HANDLE ALL OF YOUR REPAIR AND SERVICE NEEDS INCLUDING CALL US NOW!(301) 931-3300. 10111B BACOCON DRIVE,BELTSVILLE,MD 20705


Monday, May 15, 2017

Katibu Mkuu UN alaani mashambulio dhidi ya raia na wasimamia amani CAR

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa amelaani mashambulio ya hivi karibuni ya makundi ya wabeba silaha dhidi ya raia na askari wa kusimamia amani wa umoja huo MINUSCA huko katika Jamhuri ya Afrika ya Kati.

António Guterres ameeleza katika taarifa yake kwamba, shambulio dhidi ya askari wa kusimamia amani wa Umoja wa Mataifa linaweza kuhesabiwa kuwa ni jinai ya kivita.

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa amewataka viongozi wa Jamhuri ya Afrika ya Kati kuwasaka, kuwatia mbaroni na kisha kuwapandisha kizimbani wale wote waliohusika na shambulio dhidi ya askari wa UN nchini humo.

Walinda amani wanne waliuawa na wengine kadhaa kujeruhiwa kufuatia shambulio la hivi karibuni dhidi ya msafara wa askari wa kulinda amani wa Umoja wa Matiafa MINUSCA karibu na kijiji cha Yogofongo huko katika Jamhuri ya Afrika ya Kati.

Machafuko CAR yamesababisha kuongezeka wakimbizi

Wakati huo huo, Umoja wa Mataifa umesema yumkini raia zaidi ya 30 wameuawa na kundi la waasi wa Kikristo la Anti-Balaka katika mapigano yanayoendelea hivi sasa huko katika Jamhuri ya Afrika ya Kati.


Mamia ya raia wamejificha katika msikiti mmoja mjini hapo, wakihofia kuuawa na genge hilo la waasi lenye misimamo ya kufurutu ada.

Hayo yanajiri katika hali ambayo, hivi karibuni Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa llitaka kukomeshwa haraka iwezekanavyo mapigano na vitendo vya utumiaji mabavu vya makundi ya wabeba silaha huko katika Jamhuri ya Afrika ya Kati.

Chanzo: parstoday.com

No comments:

Post a Comment

Maoni yako