If you need it, we can provide: • USA 24 hours Passport service • Rush and emergency USA passport • Expedited Visa process for U.S. & foreign countries • Document Authentication •Document Legalization..For more information please contact us at: 703-286-7713

http://swahilivilla.blogspot.com/2014/01/mahojiano-na-faria-zam-kuhusu-msaada-wa.htmlKwa kuchangia chochote kile alichonacho kupitia Hilmy Disability Charity Organisation. Wasiliana na Mkurugezi wa Hilmy Disability Charity Organisation. Faria Zam. kwa UK Number ya Simu. 745-501-4372 Au Abou Shatry. U.S.A No' 301-728-3977

 http://www.dickysmallsauto.com/

DICK SMALLS AUTO MOTIVE WE CAN HANDLE ALL OF YOUR REPAIR AND SERVICE NEEDS INCLUDING CALL US NOW!(301) 931-3300. 10111B BACOCON DRIVE,BELTSVILLE,MD 20705


Saturday, May 13, 2017

KENYA: BASI LA GITHURAI 45 LAHUSIKA KATIKA AJALI NAKURU, WATU 19 WAFARIKI

Na MWANGI MUIRURI

WATU 19 wameaga dunia saa nane usiku wa kuamkia Jumamosi katika ajali ya kutamausha Kaunti ya Nakuru.

Wahudumu wa bodaboda waangalia mabaki ya basi lililogongana na lori Mei 13, 2017 eneo la Mbaruk barabara kuu ya Nakuru-Nairobi. Watu 18 walifariki papo hapo na mmoja baadaye. Picha/SILA KIPLAGAT

Katika ajali hiyo, wengine wanaokisiwa kuwa zaidi ya 40 walipata majeraha ya viwango mbalimbali na ambapo wamelazwa katika hospitali kadha za Kaunti ya Nakuru.

Kwa mujibu wa kamanda wa polisi wa Nakuru, Hassan Rashid Barua, basi la uchukuzi wa abiria lililokuwa likitoka Nairobi kuelekea Busia lilikuwa likipita trela ambapo lilikumbana na trela nyingine na kugongana ana kwa ana.

Alisema kuwa ajali hiyo ilitokea Soysambu karibu na Mbaruk ndani ya urefu wa barabara ya Nairobi kuelekea Nakuru.

“Kitu cha kwanza kuhusu ajali hii: Basi hilo limesajiliwa kuhudumu katika barabara ya Thika Superhighway kutoka Nairobi hadi Githurai 45. Tunataka kuelewa ni jinsi gani likawa katika barabara tofauti kabisa ya kutoka Nairobi hadi masafa marefu ya Busia,” amesema Barua.

Alisema kuwa basi hilo limesajiliwa kuwa katika uthibiti wa Supehighway Sacco na lilikuwa na uwezo wa kubeba abiria 51.

Barua alisema kuwa kwa sasa haijulikani dereva wa basi hilo ako wapi “na anaweza kuwa miongoni mwa walioaga au awe ametoweka. Lakini tutajua tu na tutatoa habari kamili.”


Aliongeza kuwa magari hayo yote matatu yako katika uthibiti wa maafisa wa polisi “na uchunguzi kamili utatekelezwa dhidi yao kubainisha hali ya usawa kuwa barabarani.”

Aliteta kuwa ajali hiyo huenda ilisababishwa na ukosefu wa umakinifu barabarani kwa upande wa dereva wa basi hilo la uchukuzi wa abiria kwa kuwa “haileweki ni kwa maamuzi gani alikuwa akipita gari mbele yake na kukumbana na lingine moja kwa moja.”

Alisema kuwa sheria za udereva ni kuwa “usithubutu kupita magari mengine kiholela na unapoamua kufanya hivyo, unahatarisha maisha na mali hivyo basi kuwa katika usajili wa wahaini barabarani.”

Alisema kuwa atazidi kutoa taarifa kuhusu ajali hiyo “kuwafahamisha kuhusu manusura na matokeo ya uchunguzi wetu.”

Aliwatakia waliojeruhiwa afueni ya haraka huku kwa walioaga dunia akiwatakia rehema za Mwenyezi Mungu na kwa familia za wote, nguvu tosha za Maulana kukabiliana na mshtuko wa kupoteza wapendwa wao au kutwikwa mzigo wa kuugua kwa wapendwa wengine.

No comments:

Post a Comment

Maoni yako