If you need it, we can provide: • USA 24 hours Passport service • Rush and emergency USA passport • Expedited Visa process for U.S. & foreign countries • Document Authentication •Document Legalization..For more information please contact us at: 703-286-7713

http://swahilivilla.blogspot.com/2014/01/mahojiano-na-faria-zam-kuhusu-msaada-wa.htmlKwa kuchangia chochote kile alichonacho kupitia Hilmy Disability Charity Organisation. Wasiliana na Mkurugezi wa Hilmy Disability Charity Organisation. Faria Zam. kwa UK Number ya Simu. 745-501-4372 Au Abou Shatry. U.S.A No' 301-728-3977

 http://www.dickysmallsauto.com/

DICK SMALLS AUTO MOTIVE WE CAN HANDLE ALL OF YOUR REPAIR AND SERVICE NEEDS INCLUDING CALL US NOW!(301) 931-3300. 10111B BACOCON DRIVE,BELTSVILLE,MD 20705

Thursday, May 4, 2017

KENYA: KAMUKUNJI: MBUGUA AHIARI KUMPA FURSA YUSUF HASSAN

Na SAMMY WAWERU

ALIYEKUWA mbunge wa Kamukunji Bw Simon Mbugua hatimaye 'ameachia' ushindi wake na kukubali kumpa cheti mbunge wa sasa eneobunge hilo Bw Yusuf Hassan kutetea kiti chake kwenye uchaguzi mkuu ujao.

Yusuf Hassan
Mbunge wa Kamukunji, Yusuf Hassan. Picha/MAKTABA

Mbugua amefikia uamuzi huu baada ya kufanya mashauriano na Bodi ya Uchaguzi ya Jubilee Party.

Kwenye mchujo, Mbugua alitangazwa rasmi kuwa mshindi kwenye uchaguzi huo.

Hassan alipinga matokeo ya uchaguzi huo akilalama kwamba mchujo haukuwa wa huru na haki.

Mbugua amesalimu amri na kuhiari kumuachia Bw Hassan fursa ya kutetea kiti chake cha ubunge Kamukunji katika uchaguzi mkuu ujao wa Agosti 8.

"Kufuatia hatua ya Bw Hassan kukata rufaa na kupinga matokeo ya uchaguzi wa mchujo Kamukunji, nimekubali kumuachia awanie kiti hicho katika uchaguzi mkuu ujao kwa sababu ni ndugu yetu na rafiki kutoka jamii jirani ya Somalia," amesema Mbugua leo Alhamisi katika makao makuu ya Jubilee eneo la Pangani, Nairobi kwenye kikao na wanahabari.


"Nina uhakika hata uchaguzi huo ukirudiwa hii leo bado nitaibuka mshindi lakini kwa sababu yeye ni ndugu yetu nimemuachia na nitamuunga mkono kuchaguliwa kwenye kiti hicho.

Wengi wa wafuasi wangu najua uamuzi huu utawaatua moyo, hususan wale waliogharamika kunifanyia kampeni. Tunataka tudumishe uhusiano mwema kwenye chama cha Jubilee ili tuibuke washindi kwenye kiti cha urais Agosti 8," amesema Mbugua.

No comments:

Post a Comment

Maoni yako