If you need it, we can provide: • USA 24 hours Passport service • Rush and emergency USA passport • Expedited Visa process for U.S. & foreign countries • Document Authentication •Document Legalization..For more information please contact us at: 703-286-7713

http://swahilivilla.blogspot.com/2014/01/mahojiano-na-faria-zam-kuhusu-msaada-wa.htmlKwa kuchangia chochote kile alichonacho kupitia Hilmy Disability Charity Organisation. Wasiliana na Mkurugezi wa Hilmy Disability Charity Organisation. Faria Zam. kwa UK Number ya Simu. 745-501-4372 Au Abou Shatry. U.S.A No' 301-728-3977

 http://www.dickysmallsauto.com/

DICK SMALLS AUTO MOTIVE WE CAN HANDLE ALL OF YOUR REPAIR AND SERVICE NEEDS INCLUDING CALL US NOW!(301) 931-3300. 10111B BACOCON DRIVE,BELTSVILLE,MD 20705


Thursday, May 18, 2017

KENYA: KARUA SASA ATANGAZA KUONGOZA KAMPENI DHIDI YA UFISADI

Na GEORGE MUNENE

KIONGOZI wa chama cha Narc Kenya, Martha Karua na mbunge wa Kirinyaga ya Kati, Gachoki Gitari Jumanne walitangaza kuendesha kampeni madhubuti itakayolenga kuangamiza ufisadi katika kaunti hiyo.

Kiongozi wa Narc-Kenya Bi Martha Karua akihutubu awali. Picha/MAKTABA

Bi Karua anawania ugavana huku Bw Gitari ambaye amekuwa mbunge kwa mihula miwili akiwa mgombea mwenza.

Wawili hao waliokuwa wakizungumza, baada ya kutangaza kuungana ili kushindana na Bi Waiguru, waliahidi kupambana na ufisadi katika serikali ya kaunti iwapo watachaguliwa Agosti 8. “Tutahakikisha kwamba tunakabiliana na ufisadi ili kuhakikisha uchumi katika kaunti ya Kirinyaga unanawiri” akasema Bi Karua.

Bw Gitari alimmiminia sifa Bi Karua akimtaja kuwa kiongozi mwaminifu na mwadilifu aliye na uwezo wa kukabiliana na ufisadi.

“Bi Karua ni kiongozi jasiri na mwadilifu ambaye nikiwa naye tutaweza kushinda vita dhidi ya ufisadi,” akasema.

Viongozi hao walisema wameungana huku wakiwataka wapinzani wao kujiandaa kwa ajili ya kinyang’anyiro kikali.


“Si siri tena, tumeungana na tumejiandaa kikamilifu kwa ajili ya kinyang’anyiro. Wapinzani wetu wajue kuwa sisi tuko imara,” akasema Bi Karua.

Viongozi hao waliokuwa wakizungumza mjini Sagana, Jumanne alasiri walisema watafanya kampeni kali kuhakikisha wanabwaga mpinzani wao Bi Waiguru wa chama cha Jubilee.

Chanzo: swahilihub.com

No comments:

Post a Comment

Maoni yako