If you need it, we can provide: • USA 24 hours Passport service • Rush and emergency USA passport • Expedited Visa process for U.S. & foreign countries • Document Authentication •Document Legalization..For more information please contact us at: 703-286-7713

http://swahilivilla.blogspot.com/2014/01/mahojiano-na-faria-zam-kuhusu-msaada-wa.htmlKwa kuchangia chochote kile alichonacho kupitia Hilmy Disability Charity Organisation. Wasiliana na Mkurugezi wa Hilmy Disability Charity Organisation. Faria Zam. kwa UK Number ya Simu. 745-501-4372 Au Abou Shatry. U.S.A No' 301-728-3977

 http://www.dickysmallsauto.com/

DICK SMALLS AUTO MOTIVE WE CAN HANDLE ALL OF YOUR REPAIR AND SERVICE NEEDS INCLUDING CALL US NOW!(301) 931-3300. 10111B BACOCON DRIVE,BELTSVILLE,MD 20705


Wednesday, May 10, 2017

KENYA: MSISIMKO MTANDAONI RAILA KUSEMA ANAOMBEA TAIFA JERUSALEM

Na LEONARD ONYANGO

MAOMBI ya mwaniaji wa urais wa Muungano wa National Super Alliance (NASA) Raila Odinga kwa Mungu jijini Jerusalem, Israeli, jana yalizua msisimko katika mitandao ya kijamii huku Wakenya wakitoa hisia tofauti tofauti.

Kinara wa CORD  Raila Odinga.
Kinara wa NASA Raila Odinga. Picha/MAKTABA

Bw Odinga ambaye yuko ziarani nchini Israeli, alizuru Hekalu la Sulemani lililoko jijini Jerusalem ambapo alituma maombi yake kwa Mungu kupitia kijikaratasi alichotia katika ufa ulio kwenye ukuta wa ekalu hilo.

“Wiki hii nilisafiri kuelekea katika Nchi Takatifu (Israeli) kuhutubia kongamano kuhusu Demokrasia, Dini na Amani barani Afrika. Nilipokuwa jijini Jerusalem, nilitembelea ukuta unaofahamika kama ‘Western Wall’.

Ukuta wa Western Wall ndio madhabahu ya Hekalu la Sulemani na inaaminika kwamba lilijengwa zaidi ya miaka 5,000 iliyopita,” akasema Bw Odinga kupitia ukurasa wake wa Facebook.

Hekalu hii ni sehemu takatifu ya madhehebu matatu ya uzao wa Ibrahimu ambayo ni kanisa la Juda, Waislamu na Wakristo na kwangu ni nembo ya nguvu na umoja,” akaongezea.

Kulingana na picha alizotia mlangoni, Bw Odinga alionekana akiomba huku akiwa amevalia kijikofia cheupe kichwani. Picha nyingine pia ilionyesha akitia kwenye ufa wa ukuta wa hekalu kijikaratasi alichoandika maombi yake kwa Mungu.


Inaaminika kuwa matakwa yanayoandikwa katika kijikaratasi na kutiwa kwenye ufa wa ukuta huo wa Western Wall yanamfikia Mungu moja kwa moja mbinguni.

“Unaanza kwa kuandika maombi yako kwenye kijikaratasi, kisha unakishikisha ukutani halafu unaomba na ujumbe wako unamfikia Mungu moja kwa moja,’ akasema Bw Odinga.

Kinara wa NASA, hata hivyo, hakufichua ikiwa azma yake ya kutaka kuwa rais wa Kenya, yalikuwa miongoni mwa matakwa yake ambayo alimwomba Mungu amtimizie.

“Nilianza kuandika matakwa yangu kwa Mungu kwa ajili ya taifa la Kenya nilipokuwa kizuizini kwa miaka sita (wakati wa utawala wa Rais Mstaafu Daniel Moi. Gereza ni sehemu mbovu isiyotamanika.

Unakuwa mpweke kwa saa 23 kati ya 24 na ilichukua miezi sita barua kuwafikia wapendwa wako. Tangu wakati huo nilipokuwa kizuizini, niliandika matakwa na maono yangu niliyo nayo kwa Wakenya,” akasema Bw Odinga.

“Kila mara ninapozuru Israeli napeleka baadhi ya matakwa hayo katika ukuta wa Western Wall,” akaongezea.

Picha hizo za Bw Odinga zilizua msisimko na hisia si haba miongoni mwa Wakenya katika mitandao ya Facebook na Twitter. “Amina, Mungu ndiye mpaji ukimpigia magoti bila shaka atajibu maombi yako,” akasema Soita Francis.

Motari Kemunto Faith alisema, “ Mungu ajibu maombi yako ya kuwa rais wa Kenya. Mathayo 7:7 inasema maombi yatajibiwa.”

Irungu Kimutai Moses alisema, “ Rais wangu Raila Odinga umeonyesha kwamba wewe ni Joshua wa kweli atakayeongoza Kenya Jerusalem.”

“Hata ukiomba hutachaguliwa kuwa rais ni sharti utueleze manifesto yako kwa Wakenya,” akasema Kamau James.

No comments:

Post a Comment

Maoni yako