If you need it, we can provide: • USA 24 hours Passport service • Rush and emergency USA passport • Expedited Visa process for U.S. & foreign countries • Document Authentication •Document Legalization..For more information please contact us at: 703-286-7713

http://swahilivilla.blogspot.com/2014/01/mahojiano-na-faria-zam-kuhusu-msaada-wa.htmlKwa kuchangia chochote kile alichonacho kupitia Hilmy Disability Charity Organisation. Wasiliana na Mkurugezi wa Hilmy Disability Charity Organisation. Faria Zam. kwa UK Number ya Simu. 745-501-4372 Au Abou Shatry. U.S.A No' 301-728-3977

 http://www.dickysmallsauto.com/

DICK SMALLS AUTO MOTIVE WE CAN HANDLE ALL OF YOUR REPAIR AND SERVICE NEEDS INCLUDING CALL US NOW!(301) 931-3300. 10111B BACOCON DRIVE,BELTSVILLE,MD 20705


Wednesday, May 3, 2017

KENYA: OMBI SERIKALI IWATAFUTIE MAKAO WATOTO WA KINA MAMA WALIOFUNGWA

Na JUDY MITO

MKUU wa kanisa Katoliki eneo la Magharibi, Joseph Obanyi, anairai serikali kuwatafutia makao yatayowafaa watoto waliolazimika kukaa gerezani na kina mama wao.

Obanyi Joseph
Kasisi Obanyi Joseph (vazi la zambarau) na mchungaji mkuu wa Kanisa Katoliki katika magereza nchini Kenya, Bw Peter Kimani (vazi la bluu). Picha/ISAAC WALE

Kasisi huyo alisema kuwa watoto wenye umri mchanga hawapswi kuishi katika mazingira hayo.

Aliyasema haya Jumanne alipokuwa akifungua tawi la kanisa la Kikatoliki katika gereza kuu la Kakamega.

“Watoto hawa hawana hatia yoyote na kuwekwa kizimbani kutaathiri ukuaji wao,” alisema Bw Obanyi.

Akizungumza katika hafla hiyo mchungaji mkuu wa magereza wa kanisa la katoliki Bw Peter Kimani alisema kuwa walifurahishwa na mabadiliko ya sheria ya kutowahukumu wakiukaji sheria hukumu ya kifo.

Kimani alisema kuwa hatua hiyo iliwapa wafungwa fursa ya kubadili mienendo yao na kuwapa fursa mpya ya kuishi maisha yasiyo na makosa.


“Sababu kuu ya kanisa kufunguliwa hapa gerezani ni kuwasaidia wafungwa kuchukua mkondo mwema utakao wasaidia baada ya maisha yao gerezani,” alisema Kimani.

Mkuu wa gereza hilo Bw Emase Nicolas alisema kuwa hatua ya kanisa Katoliki itawasaidia kuwarekebisha tabia wafungwa.

“Gereza hili lina wafungwa wasio na maadaili yanayokubalika na tunatumahi kwamba kupata chakula cha roho kitawabadili mienendo,” alisema Bw Emase.

Chanzo: swahilihub.com

No comments:

Post a Comment

Maoni yako