If you need it, we can provide: • USA 24 hours Passport service • Rush and emergency USA passport • Expedited Visa process for U.S. & foreign countries • Document Authentication •Document Legalization..For more information please contact us at: 703-286-7713

http://swahilivilla.blogspot.com/2014/01/mahojiano-na-faria-zam-kuhusu-msaada-wa.htmlKwa kuchangia chochote kile alichonacho kupitia Hilmy Disability Charity Organisation. Wasiliana na Mkurugezi wa Hilmy Disability Charity Organisation. Faria Zam. kwa UK Number ya Simu. 745-501-4372 Au Abou Shatry. U.S.A No' 301-728-3977

 http://www.dickysmallsauto.com/

DICK SMALLS AUTO MOTIVE WE CAN HANDLE ALL OF YOUR REPAIR AND SERVICE NEEDS INCLUDING CALL US NOW!(301) 931-3300. 10111B BACOCON DRIVE,BELTSVILLE,MD 20705

Tuesday, May 9, 2017

KFCB YAPIGA MARUFUKU MCHEZO WA MAUTI WA BLUE WHALE

Na BERNARDINE MUTANU

BODI ya kuanisha filamu nchini (KFCB) imepiga marufuku mchezo wa video wa ‘Blue Whale’ baada ya vifo kuripotiwa nchini.

Ezekiel Mutua
Afisa Mkuu Mtendaji wa Bodi ya Kudhibiti Filamu Kenya (KFCB), Ezekiel Mutua. Picha/SALATON NJAU

Bodi hiyo imetaka mchezo huo kuondolewa katika mitandao ya kijamii mara moja na kutishia kumkamata na kumfungulia mashtaka yeyote atakayepatikana kuruhusu watoto kuucheza.

Visa kadhaa vimeripotiwa ambapo wachezaji, hasa vijana wa umri mdogo, wamejitoa uhai kwa kushawishiwa na mchezo huo.

“Tumevutiwa na habari kuhusiana na mchezo wa mtandao ambao unatumiwa kuwafanya watoto kutekeleza hatua hatari kupitia kwa michezo ya siku 50 mfululizo,” alisema Mkurugenzi Mkuu wa KFCB Dkt Ezekiel Mutua Jumanne Mei 9, 2017.

Michezo ambayo imejumuishwa katika apu hiyo ya ‘Blue Whale’ ni pamoja na kutazama video ya kutisha na kujiumiza.

Sehemu ya mwisho ya mchezo huo ‘The Blue Whale Challenge’ hushinikiza mchezaji kujitoa uhai ili aweze kuwa ‘mshindi’.


Mchezo huo umeingiliana na michezo mingine kama vile ‘A Silent House’, ‘A Sea of Whale’, ‘Wake Me Up at 2.40am’, alisema Dkt Mutua, na hulenga watoto na vijana wa umri mdogo.

Katika eneo la Kamukunji, mvulana wa miaka 16 alijitoa uhai kwa kucheza mchezo huo wiki iliyopita.

Kulingana na mkurugenzi huyo, mchezo huo unaendelea kupata umaarufu nchini miongoni mwa watoto hasa katika maeneo ya mijini.

No comments:

Post a Comment

Maoni yako