If you need it, we can provide: • USA 24 hours Passport service • Rush and emergency USA passport • Expedited Visa process for U.S. & foreign countries • Document Authentication •Document Legalization..For more information please contact us at: 703-286-7713

http://swahilivilla.blogspot.com/2014/01/mahojiano-na-faria-zam-kuhusu-msaada-wa.htmlKwa kuchangia chochote kile alichonacho kupitia Hilmy Disability Charity Organisation. Wasiliana na Mkurugezi wa Hilmy Disability Charity Organisation. Faria Zam. kwa UK Number ya Simu. 745-501-4372 Au Abou Shatry. U.S.A No' 301-728-3977

 http://www.dickysmallsauto.com/

DICK SMALLS AUTO MOTIVE WE CAN HANDLE ALL OF YOUR REPAIR AND SERVICE NEEDS INCLUDING CALL US NOW!(301) 931-3300. 10111B BACOCON DRIVE,BELTSVILLE,MD 20705


Saturday, May 20, 2017

Korea Kaskazini: Marekani haina budi isipokuwa iachane na siasa za uhasama dhidi yetu

Naibu balozi wa Korea Kaskazini katika Umoja wa Mataifa amesema kuwa, sasa umefika wakati Marekani kuchanea na siasa zake za uhasama dhidi ya Pyongyang.

Kim In Ryong amesema kuwa, kabla ya Marekani kuanza mazungumzo yoyote na Korea Kaskazini, kwanza inatakiwa kuachana na siasa zake za uadui dhidi ya Pyongyang. Amesema: "Kama ambavyo kila mtu anafahamu kwamba, Washington imekusudia kufanya mazungumzo na Korea Kaskazini, lakini jambo muhimu sio maneno wala mazungumzo, bali ni vitendo." Mwisho wa kunukuu.

Kim In Ryong, Naibu balozi wa Korea Kaskazini katika Umoja wa Mataifa

Kadhalika naibu balozi wa Korea Kaskazini katika Umoja wa Mataifa amesema kuwa, kubadilika siasa za uhasama za Marekani dhidi ya Poyongyang ndilo sharti la kila kitu kwa ajili ya kutatuliwa mgogogro wa Peninsula ya Korea na kwamba, siasa hizo mbaya za Washington ndicho chanzo cha matatizo katika eneo tajwa. Wakati huo huo, meli ya kivita ya Marekani ya USS Ronald Reagan ambayo ilikuwa imetia nanga nchini Japan, imeanza safari kuelekea karibu na Korea Kaskazini.

Meli ya kivita ya Marekani ya USS Ronald Reagan


Inafaa kuashiria kuwa, katika hali ambayo Marekani inataka kufanya mazungumzo na Pyongyang, imekuwa ikiiwekea mashinikizo ikiwa ni pamoja na kuiwekea vikwazo ambapo hivi karibuni iliilazimisha China kuacha kununua makaa ya mawe yanayozalishwa Korea Kaskazini. 

Hii ni katika hali ambayo kwa mara kadhaa Pyongyang imekuwa ikisisitiza kuwa, miradi ya nyuklia na makombora yake ya balestiki ni kwa ajili ya kujilinda na mashambulizi tarajiwa ya Marekani.

Chanzo: hparstoday.com

No comments:

Post a Comment

Maoni yako