If you need it, we can provide: • USA 24 hours Passport service • Rush and emergency USA passport • Expedited Visa process for U.S. & foreign countries • Document Authentication •Document Legalization..For more information please contact us at: 703-286-7713

http://swahilivilla.blogspot.com/2014/01/mahojiano-na-faria-zam-kuhusu-msaada-wa.htmlKwa kuchangia chochote kile alichonacho kupitia Hilmy Disability Charity Organisation. Wasiliana na Mkurugezi wa Hilmy Disability Charity Organisation. Faria Zam. kwa UK Number ya Simu. 745-501-4372 Au Abou Shatry. U.S.A No' 301-728-3977

 http://www.dickysmallsauto.com/

DICK SMALLS AUTO MOTIVE WE CAN HANDLE ALL OF YOUR REPAIR AND SERVICE NEEDS INCLUDING CALL US NOW!(301) 931-3300. 10111B BACOCON DRIVE,BELTSVILLE,MD 20705

Friday, May 5, 2017

LOWASSA ‘AMFAGILIA’ UHURU KENYATTA

Na MWANDISHI WETU

DAR ES SALAAM, Tanzania

WAZIRI Mkuu wa zamani Edward Lowassa amemuonya Rais Uhuru Kenyatta wa Kenya dhidi ya muungano wa vyama vya upinzani wa Nasa akisema utakisumbua chama tawala cha Jubilee katika Uchaguzi Mkuu wa mwezi Agosti 8, 2017.

Edward Lowassa
Edward Lowassa

Waziri Mkuu wa zamani nchini Tanzania Edward Lowassa. Picha/MAKTABA

Akizungumza kwenye mahojiano na Shirika la Utangazaji la Uingereza (BBC) juzi, licha ya kusisitiza msimamo wake wa kumuunga mkono Uhuru Kenyatta kuwania urais kwa awamu ya pili, Lowassa alisema Nasa ni umoja ambao una nguvu.

“Nawapongeza Nasa kwa muungano wao. Namshauri rafiki yangu Kenyatta asipuuze muungano ule kwa sababu una nguvu na una watu wengi. Naamini hatapuuza.” Alisema Lowassa ambaye pia aligombea urais nchini akiungwa mkono na vyama vinne vya Chadema, NCCR Mageuzi, NLD na CUF vilivyounda Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa).

Lowassa alisema wakati mwingine chama kinapokuwa kimoja, kura hazitoshi ndiyo maana vingine huungana ili kuwa kitu kimoja.

“Inawezekana mnapokuwa chama kimoja kura hazitoshi kwa hiyo mnaungana na vyama vingine na kutengeneza ‘coalition’ na kama imejitengeneza vizuri mnachukua madaraka,” alisema Lowassa na kuongeza, “Niko upinzani kwa sababu maalumu ya kuing’oa CCM madarakani”.


Alipoulizwa kama Nassa wana nguvu ya kutosha ya kumn’goa Rais Kenyatta alisema hana uhakika lakini nguvu ya muungano ni kubwa.
“Wapinzani wengi tutajifunza kutoka kwao kutokana na muungano huo hasa kama watafanikiwa.”

Licha ya kubashiri ushindani mkubwa lakini aliwashauri Wakenya kuzingatia amani.

“Watangulize amani na umoja mbele wakati na baada ya uchaguzi,” alisema.

Kuhusu kumuunga mkono Kenyatta, Lowassa alisema, “Kwanza, ni wakati wa kura za maoni za vyama. Pili, ni namuamini mtu mwenyewe na tatu nataka kauli yangu isikike. Jana (Juzi) nilikuwa na wanawake wa Kenya na walifurahi sana kusikia namuunga mkono,” alisema Lowassa.

Lowassa alisema Rais Kenyatta amekuwa mmoja w viongozi wanaoonekana kupenda na kuilinda Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC).

“Tunataka viongozi viogozi wanaojali watu. Wakati EAC inaanzishwa tulidhanikkwamba ni Jumuiya ya watu na huyu ameonyesha kwamba jii ni jumuiya ya watu,” alisema.

Mbali na kumsifia, Lowassa alisema pia kwamba kwa kipindi ambacho Rais Kenyatta amekuwa madarakani amrefany kazi nzuri na ameonyesha ana uwezo, anapenda amani na maendeleo.

Lowassa alishika nafasi ya pili katika mbio za urais Tanzania akiwa amepata kura milioni 6.07 huku rais Magufuli akipata kura 8.8 milioni

Chanzo: swahilihub.com

No comments:

Post a Comment

Maoni yako