If you need it, we can provide: • USA 24 hours Passport service • Rush and emergency USA passport • Expedited Visa process for U.S. & foreign countries • Document Authentication •Document Legalization..For more information please contact us at: 703-286-7713

http://swahilivilla.blogspot.com/2014/01/mahojiano-na-faria-zam-kuhusu-msaada-wa.htmlKwa kuchangia chochote kile alichonacho kupitia Hilmy Disability Charity Organisation. Wasiliana na Mkurugezi wa Hilmy Disability Charity Organisation. Faria Zam. kwa UK Number ya Simu. 745-501-4372 Au Abou Shatry. U.S.A No' 301-728-3977

 http://www.dickysmallsauto.com/

DICK SMALLS AUTO MOTIVE WE CAN HANDLE ALL OF YOUR REPAIR AND SERVICE NEEDS INCLUDING CALL US NOW!(301) 931-3300. 10111B BACOCON DRIVE,BELTSVILLE,MD 20705


Monday, May 15, 2017

Macron asisitiza ulazima wa kubadilika siasa za ndani na nje za Ufaransa

Rais mpya wa Ufaransa Emmanuel Macron amesisitizia ulazima wa kubadilika siasa za ndani na nje za nchi hiyo.

Macron ameyasema hayo leo katika hotuba yake ya kwanza aliyotoa katika Ikulu ya Elysee na kubainisha kuwa Ufaransa imepita kipindi cha udhaifu na kwamba wakati umefika wa kuondokana na kipindi hicho.

Rais mpya wa Ufaransa amebainisha kuwa inapasa kuondokana pia na hali ya mpasuko wa ndani iliyopo na kuongeza kwamba nafasi na hadhi ya Ufaransa duniani imeshuka kutokana na kupotea imani juu ya nchi hiyo.

Macron aidha ameutaja ugaidi kuwa tatizo kuu na la msingi na kufafanua kwamba Umoja wa Ulaya unapaswa kutoa mchango wenye ufanisi zaidi kuhusiana na suala hilo.

Rai mpya wa Ufaransa Emmanuel Macron (kulia) akiamkiana na rais aliyemaliza muda wake Francois Hollande

Sambamba na kumalizika hafla ya kupokezana madaraka, rais Francois Hollande ameondoka rasmi katika Ikulu ya Elysee baada ya kumaliza kipindi chake cha miaka mitano ya urais.

Emmanuel Macron leo Jumapili ya tarehe 14 Mei 2017 ameapishwa rasmi kuwa rais mpya wa Ufaransa.


Macron anajulikana kama rais kijana zaidi katika historia ya Ufaransa na pia ni rais wa kwanza kuchaguliwa katika miongo ya karibuni na kuingia katika Ikulu ya Elysee akiwa hatokani na vyama vikuu vya siasa vya nchi hiyo.

Hatua ya kwanza inayosubiriwa kuchukuliwa na rais mpya wa Ufaransa ni kuunda serikali mpya ya nchi hiyo.

Wakati huohuo baadhi ya duru za habari zimeripoti kuwa Rais Macron mwishoni mwa wiki ijayo atatembelea vikosi vya Ufaransa vinavyohudumu nje ya nchi, uwezekano mkubwa vikiwa ni vile vilivyoko nchini Mali.../

Chanzo: parstoday.com

No comments:

Post a Comment

Maoni yako