If you need it, we can provide: • USA 24 hours Passport service • Rush and emergency USA passport • Expedited Visa process for U.S. & foreign countries • Document Authentication •Document Legalization..For more information please contact us at: 703-286-7713

http://swahilivilla.blogspot.com/2014/01/mahojiano-na-faria-zam-kuhusu-msaada-wa.htmlKwa kuchangia chochote kile alichonacho kupitia Hilmy Disability Charity Organisation. Wasiliana na Mkurugezi wa Hilmy Disability Charity Organisation. Faria Zam. kwa UK Number ya Simu. 745-501-4372 Au Abou Shatry. U.S.A No' 301-728-3977

 http://www.dickysmallsauto.com/

DICK SMALLS AUTO MOTIVE WE CAN HANDLE ALL OF YOUR REPAIR AND SERVICE NEEDS INCLUDING CALL US NOW!(301) 931-3300. 10111B BACOCON DRIVE,BELTSVILLE,MD 20705


Tuesday, May 9, 2017

Mahakimu wa Mahakama ya Rufaa Marekani waitilia shaka amri ya Trump dhidi ya wahajiri

Mahakimu wa Mahakama ya Rufaa nchini Marekani wameitilia shaka amri ya Rais wa nchi hiyo Donald Trump dhidi ya wahajiri.

Mahakimu hao wa Mahakama ya Rufaa wameeleza kutiwa shaka na madai ya Trump kwamba amri aliyotoa ya kupiga marufuku kuingia nchini humo raia wa nchi sita ambazo idadi kubwa ya watu wake ni Waislamu imetokana na hofu juu ya usalama wa taifa wa Marekani na si kwa sababu ya chuki za kidini.

Jeffrey Wall, Naibu Mwanasheria Mkuu wa Marekani ambaye amemwakilisha Trump katika Mahakama ya Rufaa ya kitengo cha nne mjini Richmond katika jimbo la Virginia, amekabiliwa na maswali magumu ya mahakimu kadhaa wa mahakama hiyo ambao waliteuliwa na marais waliopita wa Marekani kutoka chama cha Democrat.

Maandamano ya kupinga amri ya Trump, Marekani


Mahakama ya Rufaa ya kitengo cha nne ya Marekani mjini Richmond imeundwa kwa lengo la kusikiliza ombi la rufaa la serikali ya Trump dhidi ya hukumu iliyotolewa Machi 15 mwaka huu na Hakimu wa Mahakama ya Federali katika jimbo la Maryland, Theodore Chuang.

Hukumu iliyotolewa na hakimu huyo wa Mahakama ya Federali ya Maryland ilisimamisha siku moja tu baada ya kutangazwa, utekelezwaji wa amri iliyotolewa na rais wa Marekani ya kupiga marufuku raia wa nchi sita za Kiislamu kuingia nchini humo.../

Chanzo: parstoday.com

No comments:

Post a Comment

Maoni yako