If you need it, we can provide: • USA 24 hours Passport service • Rush and emergency USA passport • Expedited Visa process for U.S. & foreign countries • Document Authentication •Document Legalization..For more information please contact us at: 703-286-7713

http://swahilivilla.blogspot.com/2014/01/mahojiano-na-faria-zam-kuhusu-msaada-wa.htmlKwa kuchangia chochote kile alichonacho kupitia Hilmy Disability Charity Organisation. Wasiliana na Mkurugezi wa Hilmy Disability Charity Organisation. Faria Zam. kwa UK Number ya Simu. 745-501-4372 Au Abou Shatry. U.S.A No' 301-728-3977

 http://www.dickysmallsauto.com/

DICK SMALLS AUTO MOTIVE WE CAN HANDLE ALL OF YOUR REPAIR AND SERVICE NEEDS INCLUDING CALL US NOW!(301) 931-3300. 10111B BACOCON DRIVE,BELTSVILLE,MD 20705


Tuesday, May 23, 2017

Mahmoud Abbas: Ukaliaji ardhi wa mabavu na ujenzi wa vitongoji ndilo tatizo kuu la Wapalestina

Mahmoud Abbas, Rais wa Mamlaka ya Ndani ya Palestina amesema, tatizo kuu la Wapalestina ni ukaliaji wa mabavu na ujenzi wa vitongoji vya walowezi wa Kizayuni unaofanywa na Israel katika ardhi za Palestina.

Abbas ameyasema hayo leo katika mazungmzo na Rais Donald Trump wa Marekani huko Bait Lahm. Akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari mara baada ya mazungumzo yake na Trump, Rais wa Mamlaka ya Ndani ya Palestina amesisitiza kuwa mapigano kati ya Wapalestina na Waisraeli si ya kidini, bali tatizo la Wapalestina ni kukaliwa kwa mabavu ardhi za Palestina, kujengwa vitongoji vya walowezi na kutotambuliwa rasmi nchi ya Palestina na Israel.

Mahmoud Abbas (kushoto) na Netanyahu katika mazungumzo ya mapatano

Mahmoud Abbas amebainisha kuwa serikali yake ya Mamlaka ya Ndani inataka kufikia mapatano na utawala wa Kizayuni na kuundwa nchi mbili huru za Palestina na Israel katika ardhi za Palestina zinazokaliwa kwa mabavu.


Kuhusiana na mateka wa Kipalestina wanaoshikiliwa kwenye magareza ya utawala wa Kizayuni na ambao wamesusia kula chakula, Abbas amesema matakwa ya mateka hao ni ya kiutu na ya kiadilifu na akawatak viongozi wa utawala wa Kizayuni kuwatekelezea matakwa yao.

Baada ya safari yake ya Saudi Arabia, siku ya Jumatatu Rais Donald Trump wa Marekani aliwasili katika ardhi zinazokaliwa kwa mabavu za Palestina (Israel) na kufanya mazungumzo na Waziri Mkuu wa utawala wa Kizayuni Benjamin Netanyahu huko Tel Aviv. 

Trump leo alielekea mjini Bait Lahm ambako alikutana na kufanya mazungumzo na Mahmoud Abbas, Rais wa Mamlaka ya Ndani ya Palestina.../

Chanzo: parstoday.com

No comments:

Post a Comment

Maoni yako