If you need it, we can provide: • USA 24 hours Passport service • Rush and emergency USA passport • Expedited Visa process for U.S. & foreign countries • Document Authentication •Document Legalization..For more information please contact us at: 703-286-7713

http://swahilivilla.blogspot.com/2014/01/mahojiano-na-faria-zam-kuhusu-msaada-wa.htmlKwa kuchangia chochote kile alichonacho kupitia Hilmy Disability Charity Organisation. Wasiliana na Mkurugezi wa Hilmy Disability Charity Organisation. Faria Zam. kwa UK Number ya Simu. 745-501-4372 Au Abou Shatry. U.S.A No' 301-728-3977

 http://www.dickysmallsauto.com/

DICK SMALLS AUTO MOTIVE WE CAN HANDLE ALL OF YOUR REPAIR AND SERVICE NEEDS INCLUDING CALL US NOW!(301) 931-3300. 10111B BACOCON DRIVE,BELTSVILLE,MD 20705


Thursday, May 18, 2017

Makamu wa Rais wa Tanzania awataka polisi wanawake kuchangamkia fursa

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania amewataka askari polisi wanawake kutoka kwenye Shirikisho la Majeshi la Polisi Kusini mwa Afrika (SARPCCO) washiriki kikamilifu katika oparesheni mbalimbali ambazo zinafanyika kwenye ukanda huo kama hatua ya kukabiliana na vitendo vya uhalifu.

Samia Suluhu Hassan, amesema hayo wakati akifungua mafunzo ya siku tatu ya polisi wanawake kutoka nchi wanachama wa SARPCCO katika Ukumbi wa Kimataifa wa Mikutano wa Mwalimu Julius Nyerere jijini Dar es Salaam Tanzania.

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania pia amewahimiza askari polisi wanawake kufanya kazi kwa bidii na kujituma, hatua ambayo itawasaidia kupanda vyeo kama askari wanaume katika maeneo yao ya kazi, na kusisitiza kuwa, muda wa kulalamika kuwa hawapandishwi vyeo umeshapitwa na wakati bali kwa sasa wachape kazi na waonyeshe kuwa wanaweza majukumu yao wanayopangiwa ili waweze kupanda vyeo.

Hamad Masauni, Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani wa Tanzania

Kuhusu utendaji kazi wa polisi wanawake, Makamu wa Rais Bi Samia Suluhu Hassan amewataka polisi hao kutumia mkutano huo wa siku tatu kujadili kwa kina namna ya kuondoa changamoto hizo zinazorudisha nyuma utendaji wao wa kazi.


Amesema kama polisi wanawake wataacha majungu na kujenga umoja na mshikamano miongoni mwao watafikia malengo yao haraka hasa katika kushiriki kikamilifu katika mapambano dhidi ya vitendo vya uhalifu ikiwemo biashara ya dawa za kulevya.

Kwa upande wake, Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani Hamad Masauni amesema ana imani kubwa kuwa mafunzo hayo yatasaidia kwa kiasi kikubwa polisi hao wanawake kuimarika ipasavyo katika utendaji wao wa kazi.

Chanzo: parstoday.com

No comments:

Post a Comment

Maoni yako