If you need it, we can provide: • USA 24 hours Passport service • Rush and emergency USA passport • Expedited Visa process for U.S. & foreign countries • Document Authentication •Document Legalization..For more information please contact us at: 703-286-7713

http://swahilivilla.blogspot.com/2014/01/mahojiano-na-faria-zam-kuhusu-msaada-wa.htmlKwa kuchangia chochote kile alichonacho kupitia Hilmy Disability Charity Organisation. Wasiliana na Mkurugezi wa Hilmy Disability Charity Organisation. Faria Zam. kwa UK Number ya Simu. 745-501-4372 Au Abou Shatry. U.S.A No' 301-728-3977

 http://www.dickysmallsauto.com/

DICK SMALLS AUTO MOTIVE WE CAN HANDLE ALL OF YOUR REPAIR AND SERVICE NEEDS INCLUDING CALL US NOW!(301) 931-3300. 10111B BACOCON DRIVE,BELTSVILLE,MD 20705

Thursday, May 4, 2017

Marekani yaichokoza tena Korea Kaskazini, yafyatua kombora jipya

Katika wakati huu ambapo hali si hali huko Korea, dola la kibeberu la Marekani limefanya uchokozi mpya kwa kufanyia majaribio kombora lake la "Minuteman III" lenye uwezo wa kupiga umbali wa karibu kilomita elfu sita na 760. Hatua hiyo ya Marekani imechukuliwa huku dunia ikiwa bado haijasahau makelele mengi yaliyopigwa kufuatia Korea Kaskazini kufanyia majaribio kombora lake jipya la balestiki.

Jeshi la Anga la Marekani limetangaza kuwa, kombora hilo limefanyiwa majaribio bila ya kuwa na silaha zinazoambatanishwa nalo. Majaribio hayo yamefanyika katika kituo cha jeshi la anga cha Vandenberg, California, na baada ya kuvuka masafa ya meli elfu nne na 200 takriban kilomita elfu 6 na 760, limepiga shabaha iliyokusudiwa.

Wiki iliyopita pia jeshi la Marekani lilifanyia majaribio kombora kama hilo yaani tarehe 26 mwezi uliopita wa Aprili na duru za kijeshi za nchi hiyo zikadai kuwa lilipiga shabaha iliyokusudiwa.

Kombora la "Minuteman III" la Marekani

Katikati ya mwezi Aprili pia, Jeshi la Anga la Marekani lilifanya majaribio mengine ya anga katika jangwa la Nevada na kudai kuwa lengo la majaribio hayo ni kufanyia majaribio uwezo wa ndege zake za F-16 wa kubeba na kufyatua mabomu aina ya B-61.


Si hayo tu, lakini pia juzi Jumanne ndege za kivita za Marekani zilipaa kwa ajili ya kushiriki kwenye mazoezi ya anga yaliyozishirikisha pia Korea Kusini na Japan.

Uchokozi wa namna hii unaipa kisingizio Korea Kaskazini cha kujiimarisha kijeshi na kufanyia majaribio silaha zake zikiwemo za nyuklia.

Cha kushangaza ni kuwa, Marekani inafanya kwa uhuru majaribio ya makombora yake na silaha zake nyingine nzito na za maangamizi, lakini huwa inalalamika mno inapoona nchi nyingine nazo zinafanyia majaribio silaha zao za kujilinda na ubeberu wake.

Chanzo: parstoday.com

No comments:

Post a Comment

Maoni yako