If you need it, we can provide: • USA 24 hours Passport service • Rush and emergency USA passport • Expedited Visa process for U.S. & foreign countries • Document Authentication •Document Legalization..For more information please contact us at: 703-286-7713

http://swahilivilla.blogspot.com/2014/01/mahojiano-na-faria-zam-kuhusu-msaada-wa.htmlKwa kuchangia chochote kile alichonacho kupitia Hilmy Disability Charity Organisation. Wasiliana na Mkurugezi wa Hilmy Disability Charity Organisation. Faria Zam. kwa UK Number ya Simu. 745-501-4372 Au Abou Shatry. U.S.A No' 301-728-3977

 http://www.dickysmallsauto.com/

DICK SMALLS AUTO MOTIVE WE CAN HANDLE ALL OF YOUR REPAIR AND SERVICE NEEDS INCLUDING CALL US NOW!(301) 931-3300. 10111B BACOCON DRIVE,BELTSVILLE,MD 20705

Thursday, May 25, 2017

NASA KUWEKA MAAJENTI 5 KILA KITUO KULINDA KURA AGOSTI 8

MUUNGANO wa Upinzani (NASA) unapanga kuwaweka watu watano katika kila kituo cha kupiga kura kote nchini kuhakikisha kuwa kura zake zimelindwa.

Nasa
Viongozi wa muungano wa Nasa, Kalonzo Musyoka (kushoto) Moses Wetang'ula, Isaac Ruto, Musalia Mudavadi na Raila Odinga Aprili 27, 2017 wakiwa Uhuru Park. Picha/DENNIS ONSONGO

Kwenye mkakati huo, NASA pia imetangaza kununua kamera na zaidi ya simu 40,000 maalum ili kuewawezesha kurekodi kila matukio yanayojiri katika vituo hivyo, hasa wakati kuhesabu kura kwenye Uchaguzi Mkuu wa Agosti.

Wakiwahutubia wakazi wa Kaunti ya Isiolo mnamo Jumatano wakati wa mkutano wa kisiasa, kiongozi wa muungano huo Raila Odinga alisema kwamba hawataacha nafasi yoyote kwa “wizi wa kura kuendeshwa na serikali ya Jubilee”.

Bw Odinga, aliye pia mgombea urais, alisema watakuwa wakinakili na kutengeneza sajili yao mpya kila baada ya saa tatu, ili kuhakikisha kwamba hakuna “wageni” wanaoshiriki katika upigaji kura.

“Hakuna wageni watakaopiga kura mara hii, kinyume na walioorodheshwa katika Sajili Kuu ya Kitaifa,” akasema Bw Odinga. Mgombea mwenza Kalonzo Musyoka alisema kuwa wameziba mianya yoyote ambayo Jubilee inaweza kutumia kuiba kura.

“Tumejipanga vilivyo. Mara hii hali ni tofauti sana. Tunataka kuwaambia wenzetu Jubilee kwamba ikiwa walidhani wamerauka, sisi tushakesha na kujipanga. Hawatakuwa na nafasi yoyote ya kuwahadaa Wakenya tena,” akasema Bw Musyoka.


Aidha, Musyoka, alisema kwa simu hizo, maajenti hao watapiga picha matokeo yatakayotangazwa katika vituo hivyo, ili kuyaweka kama ushahidi ikiwa, Tume ya Uchaguzi na Mipaka (IEBC) itajaribu kuyabadilisha katika Kituo cha Kitaifa cha Kuhesabu Kura.

Wawili hao walikuwa wameandamana na vinara wenza Musalia Mudavadi (ANC), Seneta Moses Wetang’ula (Bungoma) na mwenyekiti mpya wa Baraza la Magavana (COG) Josephat Nanok, mbunge Junnet Mohammed (Suna Mashariki) kati ya wengine.

Bw Wetang’ula alimwambia Naibu Rais William Ruto kukoma kuwatukana viongozi wa NASA, huku akiifananisha Jubilee na chama cha KANU mnamo 2002 pamoja na kulinganisha NASA na uliokuwa muungano wa NARC.

Mudavadi alisema kuwa lengo lao ni kuibuka washindi kwa kishindo.

“Tunataka kuushinda uchaguzi huu katika duru ya kwanza. Tunawaomba wafuasi wetu kuamka mapema na kupiga kura zao.

Chanzo: swahilihub.com

No comments:

Post a Comment

Maoni yako