If you need it, we can provide: • USA 24 hours Passport service • Rush and emergency USA passport • Expedited Visa process for U.S. & foreign countries • Document Authentication •Document Legalization..For more information please contact us at: 703-286-7713

http://swahilivilla.blogspot.com/2014/01/mahojiano-na-faria-zam-kuhusu-msaada-wa.htmlKwa kuchangia chochote kile alichonacho kupitia Hilmy Disability Charity Organisation. Wasiliana na Mkurugezi wa Hilmy Disability Charity Organisation. Faria Zam. kwa UK Number ya Simu. 745-501-4372 Au Abou Shatry. U.S.A No' 301-728-3977

 http://www.dickysmallsauto.com/

DICK SMALLS AUTO MOTIVE WE CAN HANDLE ALL OF YOUR REPAIR AND SERVICE NEEDS INCLUDING CALL US NOW!(301) 931-3300. 10111B BACOCON DRIVE,BELTSVILLE,MD 20705


Monday, May 1, 2017

Onyo kali la China kwa Marekani kuhusu kuanzisha vita dhidi ya Korea Kaskazini

Waziri wa Mambo ya Nje wa China Wang Yi ameionya Marekani kutochukua hatua yoyote ya ya kichokozi dhidi ya Korea Kaskazini.

Akizungumza katika mahojiano pembeni ya kikao cha Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa kilichozungumzia kadhia ya Korea Kaskazini Wang Yin amesisitiza kuwa kutokana na mstari mwekundu uliowekwa na China, nchi hiyo haitoruhusu Marekani na Korea Kusini ziingie vitani dhidi ya Korea Kaskazini.

Waziri wa Mambo ya Nje wa China, Wang Yi

Huku akisisitiza kuhusu uelewa kamili walionao juu ya hali tete na hasasi iliyopo katika eneo la Peninsula ya Korea, Waziri wa Mambo ya Nje wa China amesema, kinachohitajika ni kuanza mara moja mazungumzo ya nyuklia ya pande sita mjini Beijing na kuipa uzito kwa maana halisi diplomasia na mazungumzo kwa ajili ya kutatua mgogoro wa eneo hilo.

Sambamba na matamshi hayo ya Wang Yi, Wizara ya Mambo ya Nje ya China pia imetoa taarifa ikizitaka pande zote ziwe na stahamala na kutoifanya hali ya mambo iwe mbaya zaidi.

Maneva ya pamoja ya Marekani na Korea Kusini

Msimamo mkali ulioonyeshwa na Waziri wa Mambo ya Nje wa China kwamba Beijing haitaruhusu Marekani na Korea Kusini zianzishe vita dhidi ya Korea Kaskazini, ni onyo na indhari kali zaidi kuwahi kutolewa na China kwa Washington na Seoul kuhusiana na masuala ya Peninsula ya Korea na mzozo wa pande hizo mbili na Pyongyang.


Onyo hilo limetolewa baada ya baadhi ya maafisa wa Marekani kutangaza kuwa ni vigumu kupata njia mwafaka ya kidiplomasia kwa ajili ya kutatua kadhia ya nyuklia katika Peninsula ya Korea.

Msimamo ngangari ulioonyeshwa na Waziri wa Mambo ya Nje wa China kwamba nchi yake haitaruhusu Marekani na Korea Kusini zianzishe vita dhidi ya Korea Kaskazini umefikisha ujumbe kwa nchi hizo mbili kuwa kama zinataka kuanzisha vita katika Peninsula ya Korea zijue kwamba Beijing itakuwa bega kwa bega na Pyongyang.

Onyo hilo ambalo halijawahi kushuhudiwa, limetolewa na China kwa Marekani katika hali ambayo tangu Donald Trump aingie madarakani mwezi Januari mwaka huu, Ikulu ya Marekani White House imekuwa ikipinga kila jitihada na wito ambao serikali ya Beijing imetoa kwa ajili ya kutatua kwa njia za amani mgogoro wa Peninsula ya Korea .

Na hasa ikizingatiwa kuwa hivi karibuni jeshi la Marekani limetuma Peninsula ya Korea manowari zake za kisasa ambayo ni ishara ya kutaka kuanzisha sokomoko katika eneo hilo, mbali na hatua yake ya kufanya maneva ya pamoja na nchi za Japan na Korea Kusini katika peninsula hiyo.

Manowari ya Marekani ikielekea Peninsula ya Korea

Kwa hakika msimamo uliotangazwa na Waziri wa Mambo ya Nje wa China umeonyesha kuwa nchi hiyo haitaki ionekane mtazamaji tu wa sera za kuwasha moto wa chokochoko na wa hatua haribifu za Marekani kuhusiana na kadhia za nyuklia na makombora za Korea Kaskazini; hatua ambazo zinahatarisha amani na usalama wa mashariki ya Asia na hata nje ya eneo hilo.

Onyo na indhari ya Wang Yi inabeba ujumbe huu, kwamba China ni mdau hai na amilifu katika matukio ya eneo la Peninsula ya Korea; na kutokana na malengo yake ya kistratejia itasimama kukabiliana na hatua yoyote ya kushupalia vita itakayochukuliwa na Marekani na Korea Kusini dhidi ya Korea Kaskazini.

China, ambayo inavichukulia vita vyovyote vinavyoweza kuanzishwa na Marekani na Korea Kusini dhidi ya Korea Kaskazini kuwa tishio kubwa kwa maslahi yake ya kitaifa na ya kieneo, imetoa onyo hilo ili kujaribu kuibana Marekani irudi nyuma katika mipango yake ya kuzusha chokochoko katika Peninsula ya Korea.

Jaribio la kombora lililofanywa na Korea Kaskazini

Hii ni pamoja na kuwa viongozi wa Beijing wameishauri mara kadhaa serikali ya Korea Kaskazini isimamishe shughuli zake za makombora na za nyuklia ili kuifunga mikono Marekani isipate kisingizio cha kuwasha moto wa vita katika eneo hilo.

Matarajio ya China baada ya kuitangazia Washington na Seoul kinagaubaga mismamo wake kuhusu hatua ya kutaka kuanzisha vita dhidi ya Pyongyang, ni kuziona pande mbili hizo zikichukua hatua ya kufufua mazungumzo ya pande sita ya nyuklia, kama chaguo bora la kutatua kadhia ya nyuklia ya Korea Kaskazini.

No comments:

Post a Comment

Maoni yako