If you need it, we can provide: • USA 24 hours Passport service • Rush and emergency USA passport • Expedited Visa process for U.S. & foreign countries • Document Authentication •Document Legalization..For more information please contact us at: 703-286-7713

http://swahilivilla.blogspot.com/2014/01/mahojiano-na-faria-zam-kuhusu-msaada-wa.htmlKwa kuchangia chochote kile alichonacho kupitia Hilmy Disability Charity Organisation. Wasiliana na Mkurugezi wa Hilmy Disability Charity Organisation. Faria Zam. kwa UK Number ya Simu. 745-501-4372 Au Abou Shatry. U.S.A No' 301-728-3977

 http://www.dickysmallsauto.com/

DICK SMALLS AUTO MOTIVE WE CAN HANDLE ALL OF YOUR REPAIR AND SERVICE NEEDS INCLUDING CALL US NOW!(301) 931-3300. 10111B BACOCON DRIVE,BELTSVILLE,MD 20705

Monday, May 29, 2017

RAUNDI HII NI KIMBUNGA KIKALI KULIKO TSUNAMI YA 2002 - RAILA

Na WANDERI KAMAU

KINARA wa NASA Raila Odinga amesema kwamba wimbi la sasa la muungano huo ni dhoruba kali, hata kuliko 'Tsunami’ ya muungano wa Narc mnamo 2002.

Raila Odinga a
MWANIAJI urais wa muungano wa NASA Bw Raila Odinga ahutubu Mei 28, 2017 jijini Nairobi baada ya IEBC kukubali stakabadhi zake za kuwania urais Agosti 8, 2017. Picha/ HISANI

Bw Odinga alisema kuwa kinyume na awali, wamejitayarisha vilivyo kutwaa ushindi, “kwani ni dhahiri kwamba asilimia kubwa ya Wakenya wameamua kutuunga mkono”.

Akiwasilisha stakabadhi zake za uteuzi kwa Tume Huru ya Uchaguzi na Mipaka (IEBC) katika Jumba la Mikutano la KICC, jijini Nairobi jana, Odinga alisema kuwa ni wazi kwamba muungano wa Jubilee hauna lolote kwa sasa, kwani umewafeli Wakenya kutokana na msururu wa changamoto zinazowakumba.

“Tsunami ya sasa ni dhoruba kali, litalaoutikisa ulingo wa siasa nchini. Wimbi la 2002 lilikuwa kionjo tu; mambo ni kangaja huenda yakaja. Wakati wa Jubilee kwenda nyumbani umefika,” akasema Bw Odinga kwenye kikao na wanahabari, baada ya kupokea cheti cha kuwania urais kutoka kwa mwenyekiti wa IEBC Wafula Chebukati.

Aliandamana na mgombea mwenza Kalonzo Musyoka (Wiper), wenzake Musalia Mudavadi (ANC), Gavana wa Bomet Isaac Ruto (CCM) na Seneta Moses Wetang’ula (Ford Kenya).

Hata hivyo, Bw Odinga alieleza wasiwasi kuhusu kuendelea kutumika kwa vikosi vya usalama na serikali, akitaja hilo kama hali inayozua wasiwasi kuhusu ikiwa Uchaguzi Mkuu wa Agosti utakuwa huru na wenye haki.


“Nina wasiwasi kuhusu matumizi ya vikosi vya usalama, kwani hii inaonekana kama njama ya kuwakabili wale wanaoonekana kuwa wapinzani wakuu wa serikali,” akasema Bw Odinga, akiongeza kuwa watakubali matokeo ya uchaguzi huo ikiwa tu yatakuwa huru na ya haki.

Kwa upande wake, Bw Musyoka aliilaumu serikali ya Jubilee kwa kuwatumia mawaziri na machifu kuifanyia kampeni Serikali.

“Tunataka kuwaambia Jubilee kwamba machifu nchini si wao pekee, ili kuwatumia kuendeleza kampeni zao. Tutachukua hatua za kisheria ikiwa hili litaendelea,” akasema Bw Musyoka.

Kama onyo kwa wawaniaji, Bw Chebukati alisema kwamba watakuwa macho, ili kumkabili mwaniaji yeyote ambaye ataendesha matamshi ya chuki.

“Tutakuwa macho. Hatutasita kumpiga marufuku mwaniaji yeyote ambaye tutahisi anakiuka kanuni za Sheria ya Uchaguzi, ambapo anatakiwa kuzingatia amani,” akasema.

Awali, tume hiyo ilimpa cheti mwaniaji wa muungano wa Thirdway Alliance, Dkt Ekuru Aukot, aliyeahidi kuleta mwamko mpya katika uongozi.

Hata hivyo, mwenzake Abdouba Dida (Alliance for Real Change) alilazimika kuwasilisha upya stakabadhi zake, baada ya kubainika kuwa cheti cha shahada yake ya chuo kikuu hakikuwa kimeidhinishwa na chuo.

Ilimlazimu kuwasili baadaye ndipo akapewa cheti chake.

Mwingine aliyepewa cheti cha kuwania ni Justus Juma (Justice and Freedom Party).

Chanzo: swahilihub.com

No comments:

Post a Comment

Maoni yako