If you need it, we can provide: • USA 24 hours Passport service • Rush and emergency USA passport • Expedited Visa process for U.S. & foreign countries • Document Authentication •Document Legalization..For more information please contact us at: 703-286-7713

http://swahilivilla.blogspot.com/2014/01/mahojiano-na-faria-zam-kuhusu-msaada-wa.htmlKwa kuchangia chochote kile alichonacho kupitia Hilmy Disability Charity Organisation. Wasiliana na Mkurugezi wa Hilmy Disability Charity Organisation. Faria Zam. kwa UK Number ya Simu. 745-501-4372 Au Abou Shatry. U.S.A No' 301-728-3977

 http://www.dickysmallsauto.com/

DICK SMALLS AUTO MOTIVE WE CAN HANDLE ALL OF YOUR REPAIR AND SERVICE NEEDS INCLUDING CALL US NOW!(301) 931-3300. 10111B BACOCON DRIVE,BELTSVILLE,MD 20705


Wednesday, May 10, 2017

Sisitizo la Putin la kuendeleza mapambano dhidi ya ugaidi, misimamo mikali na unazi mambo leo

Rais Vladimir Putin wa Russia alisema katika hotuba aliyoitoa jana Jumanne kwa mnasaba wa Siku ya Ushindi mjini Moscow kwamba kuna udharura kwa jamii ya kimataifa kusimama imara na kushirikiana kukabiliana na vitisho vinavyohatarisha usalama wa wote. 

Amesema, kuna udharura wa kuweko mapambano ya kweli dhidi ya ugaidi, misimamo mikali, unazi mambo leo na kila kitu kinachohatarisha usalama wa kimataifa. Aidha amesema, Moscow iko tayari kushirikiana na nchi yoyote ile katika jambo hilo.

Hatua ya Putin ya kusisitizia tena wajibu wa kupambana na mgogoro mkubwa wa kiusalama duniani hususan ugaidi, misimamo mikali na unazi mambo leo yametolewa katika wakati huu ambapo migogoro hiyo imeongezeka sana na kuhatarisha maisha ya watu katika maeneo tofauti duniani. 

Wachambuzi wa mambo wanasema kuwa, hatua ya Rais wa Russia ya kutoa matamshi hayo katika seherehe za ushindi wa nchi hiyo dhidi ya Ujerumani ya Kinazi, inaonesha ni kiasi gani Putin analipa umuhimu suala hilo la kupambana na mambo yanayohatarisha usalama duniani. 

Alaakullihaal, sasa hivi kuna baadhi ya maeneo duniani yanashuhudia kwa kiwango kikubwa zaidi vitendo vya kigaidi na misimamo ya kufurutu ada. Hivi sasa nchi za Syria na Iraq zimo latika vita vikubwa vya kupambana na magenge ya kigaidi.

Mwanajeshi wa Syria akipachika bendera ya ushindi ya nchi yake baada ya kukomboa moja ya maeneo muhimu

Kwa upande wake, Russia inasaidiana na serikali ya Syria kuendesha vita hivyo kutokana na kuamini kwamba, ugaidi ni donda ndugu la kensa ambalo likiachiwa, huenea na kuuangamiza mwili mzima. 


Vitendo vya kigaidi vya hivi karibuni vilivyotokea huko Saint Petersburg nchini Russia vimezidi kuamsha hisia za viongozi wa Moscow za wajibu wa kushirikiana na nchi nyingine kuendesha vita dhidi ya ugaidi. 

Kwa miaka mingi sasa Russia imekuwa ikipambana na magenge ya wakufurishaji na yenye misimamo mikali ndani ya ardhi ya nchi hiyo. Hadi hivi sasa magenge hayo yameshafanya vitendo kadhaa vya kigaidi ndani ya Russia. Hali hiyo imewafanya viongozi wa Russia hususan Rais wa nchi hiyo, Vladimir Putin wapate yakini kwamba haiwezekani kupambana vilivyo na ugaidi ambao unatokana na misimamo ya kuchupa mipaka na ambao unazidi kuongezeka na kupanua wigo wa maeneo yake siku baada ya siku katika kona mbalimbali za dunia bila ya kuweko ushirikiano wa mataifa yote ya dunia. 

Kwa kweli si jambo la kushangaza kuwaona viongozi wa Russia wanasisitizia mno wajibu wa kushirikiana dunia nzima kupambana vilivyo na misimamo ya kufurutu ada ambayo hatimaye huzalisha ugaidi unaohatarisha usalama wa dunia yote. Mara kwa mara Rais Vladimir Putin wa Russia amekuwa akitilia mkazo udharura wa kupambana na vyanzo vyenyewe vya ugaidi akisema kuwa, dunia haiwezi kuwa salama madhali mambo yanayochochea ugaidi yangali na nguvu. Kwa mtazamo wa weledi wa mambo, moja ya njia za kupambana na mambo yanayochochoea ugaidi ni kukabiliana na itikadi na fikra wanazojengeka nazo watu wanaotumbukia kwenye shimo la kufanya vitendo vya kigaidi.

Magaidi wanachinja watu hadharani wanadaiwa na Marekani na nchi za Magharibi na vibaraka wao kuwa eti ni waasi wenye misimamo ya wastani

Hii ni katika hali ambayo, hivi sasa Syria imegeuzwa uwanja wa kujaribia utekelezaji wa kivitendo wa itikadi na fikra za kuchupa mipaka. Cha kusikitisha ni kuwa nchi za Magharibi zinaamiliana kindumilakuwiki la hatari hiyo inayotishia usalama wa dunia nzima. Kwa mtazamo wa madola ya Magharibi yakiongozwa na Marekani, mtu anakuwa gaidi pale tu anaposhambulia nchi za Magharibi au kuua raia wa Magharibi. Lakini mtu huyo huyo anahesabiwa na madola ya Magharibi kuwa ni shujaa na mkombozi wakati anapofanya jinai na vitendo vya kigaidi dhidi ya watu wanaochukiza mbele ya Wamagharibi na vitimbakwiri vyao. Wakati huo, badala ya kupambana na magenge hayo, nchi hizo za Magharibi ikiwemo Marekani, zinaamua kuyaunga mkono kwa kila hali makundi hayo ya kigaidi na huwa tayari hata kuyatangaza hadharani kuwa eti ni waasi wenye misimamo ya wastani. Kichekesho kikubwa kingine ni kwamba, magenge hayo ya kigaidi huonekana ni matakatifu mbele ya Wamagharibi pale yanapojibadilisha jina tu. Undumilakuwili huo unashuhudiwa kwa uwazi zaidi nchini Syria sasa hivi.

Watu wenye chuki na wageni na wenye misimamo ya unazi mambo leo wanazidi kupata nguvu katika nchi za Magharibi ikiwemo Marekani

Lakini pia, hatari ya usalama duniani haiko tu upande wa misimamo mikali na ugaidi, kwani hivi karibuni katika baadhi ya nchi za Ulaya kama vile Ujerumani na Uingereza, magenge ya unazi mambo leo yenye chuki za utaifa, yameonakana yakizidi kuongezeka. 

Chuki dhidi ya wageni katika nchi za Magharibi na Marekani zinaonekana kuzidi kupata nguvu kiasi kwamba, hata wakati wa upigaji kura, watu wenye misimamo hiyo mikali ya utaifa na unazi mambo leo imma hupata ushindi au huonekana tishio kutokana na kuongezeka idadi ya wafuasi wao. 

Inaonesha Rais Vladimir Putin ameliona hilo kwa uwazi ndio maana ameamua kutumia fursa ya maadhimisho ya Siku ya Ushindi huko Russia kutoa mwito kwa jamii ya kimataifa kuunganisha pamoja nguvu zake na kupambana kikweli na kwa nia njema na ugaidi, misimamo mikali na unazi mambo leo.

Chanzo: parstoday.com

No comments:

Post a Comment

Maoni yako