If you need it, we can provide: • USA 24 hours Passport service • Rush and emergency USA passport • Expedited Visa process for U.S. & foreign countries • Document Authentication •Document Legalization..For more information please contact us at: 703-286-7713

http://swahilivilla.blogspot.com/2014/01/mahojiano-na-faria-zam-kuhusu-msaada-wa.htmlKwa kuchangia chochote kile alichonacho kupitia Hilmy Disability Charity Organisation. Wasiliana na Mkurugezi wa Hilmy Disability Charity Organisation. Faria Zam. kwa UK Number ya Simu. 745-501-4372 Au Abou Shatry. U.S.A No' 301-728-3977

 http://www.dickysmallsauto.com/

DICK SMALLS AUTO MOTIVE WE CAN HANDLE ALL OF YOUR REPAIR AND SERVICE NEEDS INCLUDING CALL US NOW!(301) 931-3300. 10111B BACOCON DRIVE,BELTSVILLE,MD 20705


Monday, May 22, 2017

Tanzania na Uganda zapiga hatua katika mradi wao wa bomba la mafuta

Marais John Pombe Magufuli wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Yoweri Museveni wa Uganda wametiliana saini tamko la pamoja la kukamilika kwa utekelezaji wa mradi wa bomba la mafuta ghafi kati ya nchi hizo mbili.

Akizungumza baada ya kutia saini tamko hilo, Rais Magufuli alimshukuru Rais Museveni kwa hatua ambayo Tanzania na Uganda zimefikia katika mradi wa bomba hilo la mafuta. 

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania amesema kuwa, mradi huo ni matokeo ya urafiki na udugu wa kihistoria uliopo kati ya nchi hizo mbili. Rais Magufuli aidha amesema, mradi huo utakuwa na manufaa makubwa kwa nchi za Uganda, Tanzania, Afrika Mashariki na Afrika nzima.

Alitaja sababu za bomba hilo kupitia Tanzania kuwa ni uwepo wa amani, uzoefu wa Tanzania katika uendeshaji wa miradi ya mabomba ya mafuta na gesi, jiografia nzuri ya usafirishaji mafuta, ardhi na ubora wa bandari ya Tanga.

Mradi wa bomba la mafuta ghafi kati ya Tanzania na Uganda

Kadhalika Rais Magufuli amesema kwamba, mradi huo utazinufaisha nchi za Afrika Mashariki yakiwemo mashirika ya ndege ambayo yatapata mafuta kwa gharama nafuu na hivyo kukua zaidi kibiashara.


Ujenzi wa mradi wa bomba la mafuta ghafi la Hoima–Tanga wenye urefu wa kilometa 1,443 zikiwemo 1,115 zitakazojengwa ndani ya ardhi ya Tanzania, utagharimu dola za Marekani bilioni 3.55. 

Hafla ya kutia saini tamko hilo ilifanyika jana Ikulu, Dar es Salaam na kuhudhuriwa na viongozi mbalimbali wa nchi zote mbili wakiwemo mawaziri, makatibu wakuu, wanasheria wakuu wa serikali, wakurugenzi na viongozi wa taasisi mbalimbali zinazohusika katika mradi huo.

Chanzo: parstoday.com

No comments:

Post a Comment

Maoni yako