If you need it, we can provide: • USA 24 hours Passport service • Rush and emergency USA passport • Expedited Visa process for U.S. & foreign countries • Document Authentication •Document Legalization..For more information please contact us at: 703-286-7713

http://swahilivilla.blogspot.com/2014/01/mahojiano-na-faria-zam-kuhusu-msaada-wa.htmlKwa kuchangia chochote kile alichonacho kupitia Hilmy Disability Charity Organisation. Wasiliana na Mkurugezi wa Hilmy Disability Charity Organisation. Faria Zam. kwa UK Number ya Simu. 745-501-4372 Au Abou Shatry. U.S.A No' 301-728-3977

 http://www.dickysmallsauto.com/

DICK SMALLS AUTO MOTIVE WE CAN HANDLE ALL OF YOUR REPAIR AND SERVICE NEEDS INCLUDING CALL US NOW!(301) 931-3300. 10111B BACOCON DRIVE,BELTSVILLE,MD 20705


Tuesday, May 2, 2017

Trump: Nipo tayari kukutana na Kiongozi wa Korea Kaskazini

Huku mgogoro ukiendelea kushtadi kati ya Marekani na Korea Kaskazini, Rais Donald Trump wa Marekani amesema kuwa, yupo tayari kukutana na kiongozi wa Korea Kaskazini, Kim Jong-un.

Trump ameyasema hayo katika mahojiano na jarida la Bloomberg na kusema kuwa, ikiwa atakutana na Kiongozi wa Korea Kaskazini, Kim Jong-un hiyo itakuwa fakhari kubwa kwake. 

Amesisitiza kuwa, ikiwa kutaandaliwa mazingira kwa ajili ya mkutano huo, yeye yupo tayari kabisa kukutana na kiongozi huyo kijana wa Korea Kaskazini.

Trump na Kim Jong-un

Rais Donald Trump ameongeza kuwa na hapa ninamnukuu: “Wanasiasa wengi hawawezi kuzungumza matamshi kama haya, lakini mimi ninasema wazi kwamba, nitakutana na Kim Jong-un ikiwa kutaandaliwa mazingira.” Mwisho wa kunukuu. 

Rais Donald Trump wa Marekani ametamka hayo katika hali ambayo, harakati za kijeshi za Washington katika Peninsula ya Korea, zimeshadidisha mgogoro katika eneo hilo kiasi cha kuifanya serikali ya Korea Kaskazini kuongeza harakati zake za silaha za nyuklia na makombora ya balestiki kwa ajili ya kukabiliana na vitisho hivyo vya Marekani. 


Hii ni katika hali ambayo, kwa mara nyingine serikali ya Korea Kaskazini imeitahadharisha Marekani kwamba, ikiwa meli za kivita za nchi hiyo zitaendelea kukaribia maji yake katika Peninsula ya Korea, basi itaziangamiza silaha za nyuklia za Washington na kuzigeuza kuwa vyuma chakavu.

Kim Jong-un, Kiongozi wa Korea Kaskazini

Katika hatua nyingine, Pyongyang imetangaza kuwa, katika kufuatilia siasa za uhasama za Marekani na washirika wake, hususan Korea Kusini na Japana, imekusudia kujizatiti kwa silaha za nyuklia ili isiweze kushambuliwa kama ilivyoshambuliwa nchi ya Syria. Kwa mujibu wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Korea Kaskazini, Pyongyang imeazimia kuunda kwa haraka sana silaha nyingi za nyuklia ili kukabiliana na vitisho vya Marekani.

Chanzo: parstoday.com

No comments:

Post a Comment

Maoni yako