If you need it, we can provide: • USA 24 hours Passport service • Rush and emergency USA passport • Expedited Visa process for U.S. & foreign countries • Document Authentication •Document Legalization..For more information please contact us at: 703-286-7713

http://swahilivilla.blogspot.com/2014/01/mahojiano-na-faria-zam-kuhusu-msaada-wa.htmlKwa kuchangia chochote kile alichonacho kupitia Hilmy Disability Charity Organisation. Wasiliana na Mkurugezi wa Hilmy Disability Charity Organisation. Faria Zam. kwa UK Number ya Simu. 745-501-4372 Au Abou Shatry. U.S.A No' 301-728-3977

 http://www.dickysmallsauto.com/

DICK SMALLS AUTO MOTIVE WE CAN HANDLE ALL OF YOUR REPAIR AND SERVICE NEEDS INCLUDING CALL US NOW!(301) 931-3300. 10111B BACOCON DRIVE,BELTSVILLE,MD 20705


Saturday, May 20, 2017

UHURU AWATAKA VIONGOZI WA NASA KUACHA KUTISHA IEBC

Na SAMMY WAWERU na MWANGI MUIRURI

VITISHO kwa Tume Huru ya Uchaguzi na Mipaka (IEBC) na mahakama inaonyesha nyinyi ni waoga na mna tabia za udikteta, Rais Kenyatta ameeleza viongozi wa National Super Alliance (Nasa).

Uhuru Kenyatta
Rais Uhuru Kenyatta akiwa na kiongozi wa Democratic Party of Kenya (DP) Joseph Munyao (kulia) Mei 19, 2017. Picha/PSCU

Rais ameusuta Nasa akisema vitisho vyake kwa IEBC na mahakama kwamba iwapo matakwa yao hayataheshimiwa hawatashiriki kwenye uchaguzi mkuu ujao wa Agosti 8 akisema hiyo inadhihirisha wao ni waoga na hawakumbatii demokrasia.

Rais amesema demokrasia ni kuwapa wananchi fursa wachague kiongozi ama viongozi wanaotaka wala si kwa kutishia tume ya IEBC na mahakama.

"Tunataka tuheshimiane, lakini si kuenda kutishia IEBC na mahakama. Vitisho hivyo vinaonyesha nyinyi ni waoga na hamna demokrasia. Demokrasia ni kuwapa wananchi fursa wachague viongozi wanaotaka wala si kutishia IEBC na korti," amesema Rais Kenyatta leo Ijumaa akilenga mrengo wa NASA kwenye kongamano la chama cha DP Nairobi kilichotangaza rasmi kuunga Rais kuchaguliwa tena kwa awamu ya pili na ya mwisho mnamo Agosti 8.

Mrengo wa upinzani NASA unaoongozwa na kinara wake Raila Odinga wa ODM akisaidiwa na mgombezi mwenza Kalonzo Musyoka wa chama cha Wiper, umeshikilia endapo matokeo ya uchaguzi mkuu wa Agosti 8 hayatatangazwa katika kiwango cha maeneo bunge hawatakuwa na budi ila kususia kushiriki uchaguzi huo wakiongeza kuwa uchaguzi huo hautafanyika.


Kwa upande wake Rais Kenyatta amesema vitisho hivyo vya NASA kwa IEBC na mahakama huenda vikayumbisha amani ya taifa.

"Watu waombe kura kwa amani wala si kwa kutishia IEBC na mahakama. Iwapo unaamini watu wanataka ajenda zako hufai kutumia vitisho unapoomba kura," Rais amesema.

Kiongozi huyu wa taifa amesema hatasita kuendesha kampeni zake kwa msingi wa kuunganisha wananchi kutoka matabaka yote nchini, kuboresha maisha ya wananchi kando na kukuza demokrasia nchini.

"Iwapo tutaendelea kuishi kwa amani na utangamano, tutakua pakubwa kimaendeleo na hasa katika sekta ya uchumi."

Chama cha DP kilicho chini ya kiongozi wake Joseph Munyao kimesema kitaunga mkono kuchaguliwa tena kwa Rais Kenyatta Agosti 8 kwa sababu ya utendakazi wake bora nchini kwa kipindi ambacho amekuwa usukani tangu serikali ya Jubilee ichaguliwe mwaka wa 2013 akisaidiwa na naibu wake William Ruto.

"Tumetazama na kufurahishwa na utendakazi wa Rais Kenyatta na serikali yake na ndio maana tukaamua kumuunga mkono achaguliwe tena. Vitisho vya upinzani NASA vinatishia demokrasia ya nchi," amesema Bw Munyao kwenye kongamano hilo la wajumbe wa chama cha DP kuunga Rais Kenyatta kuchaguliwa tena.

Mwaka wa 2002 Rais Mstaafu Mwai Kibaki alichaguliwa kuwa rais chini ya chama cha DP.
Akumbatia wagombea wanaomuunga mkono Rais ameonyesha dalili za wazi kuwa huenda akumbatie wawaniaji wote wa vyama vinavyomuunga mkono katika harakati zake za kusaka awamu ya pili ikulu.

Huku msimamo mkali wa kuonekana kupendelea wawaniaji wa Jubilee Party (JP) pekee katika kampeni za kuwadia kwa uchaguzi wa Agosti 8, 2017 ukionekana kumkwamilia Naibu wake, William Ruto Rais ameonekana kuwa kivyake katika suala hilo.

Akihutubia kongamano la chama cha Democratic Party kilichomwidhinisha kuwa mgombea wa urais ambaye kitaunga mkono, Rais Kenyatta alisema kuwa “ikiwa tunalenga lengo moja sioni ni kwa nini tuwe na mvutano.”

Alishikilia kuwa siasa za kufaa ni zile zinazoleta heshima miongoni mwa vyama vya kisiasa na pia heshima miongoni mwa wawaniaji.

“Sioni ni kwa nini kuwe na mtafaruku kati yetu katika kuafikia malengo ya kuboresha maisha ya Wakenya. Hatuwezi kuwa kwa safari moja na tuwe tunapigana. Tutashirikiana na Mungu akitujalia, tutapata ushindi tena na tuendelee mbele pamoja,” alisema.

Thibitisho la ikiwa Rais kwa uhakika ameamua kuwakumbatia wote wanaompigia debe ndani ya kampeni zake litadhihirika Jumamosi ikiwa atatii mwaliko wa wawaniaji wa kujitegemea katika uwanja wa Safaricom, Kasarani.

Wawaniaji hao wanaojumuisha gavana wa Kiambu William Kabogo, mwenzake wa Nakuru Kinuthia Mbugua na kuwa na mwenyekiti George Nyanja utakongamana kutangaza hatua za kumuunga mkono Rais Kenyatta.

Hata hivyo, katika hotuba yake ya kongamano la DP, rais hakutaja uwaniaji kwa tiketi ya kutoegemea chama bali alionekana kuunga mkono ushirika wa walio na vyama thabiti na vinavyotambulika.

Kando na DP, vyama vilivyotangaza rasmi kuunga mkono Rais Kenyatta kuchaguliwa tena kwa awamu ya pili na ya mwisho ni: KANU cha Gedion Moi, Maendeleo Chap Chap MCC cha Gavana wa Machakos Dkt Alfred Mutua, Narc Kenya cha Martha Karua, Frontier Alliance Party (FAP) na Economic Freedom Party.

Chanzo: swahilihub.com

No comments:

Post a Comment

Maoni yako