If you need it, we can provide: • USA 24 hours Passport service • Rush and emergency USA passport • Expedited Visa process for U.S. & foreign countries • Document Authentication •Document Legalization..For more information please contact us at: 703-286-7713

http://swahilivilla.blogspot.com/2014/01/mahojiano-na-faria-zam-kuhusu-msaada-wa.htmlKwa kuchangia chochote kile alichonacho kupitia Hilmy Disability Charity Organisation. Wasiliana na Mkurugezi wa Hilmy Disability Charity Organisation. Faria Zam. kwa UK Number ya Simu. 745-501-4372 Au Abou Shatry. U.S.A No' 301-728-3977

 http://www.dickysmallsauto.com/

DICK SMALLS AUTO MOTIVE WE CAN HANDLE ALL OF YOUR REPAIR AND SERVICE NEEDS INCLUDING CALL US NOW!(301) 931-3300. 10111B BACOCON DRIVE,BELTSVILLE,MD 20705

Thursday, May 25, 2017

Wakili binafsi wa Trump kuongoza jopo lake la utetezi katika faili la "Trump- Russia"

Rais Donald Trump wa Marekani amemwajiri wakili wake wa binafsi Marc Kasowitz kuongoza jopo lake la utetezi dhidi ya tuhuma zinazomkabili za kuwepo mahusiano baina ya timu yake ya kampeni za uchaguzi na maafisa wa serikali ya Russia.

Duru za kuaminika zinaeleza kuwa Trump jana alimteua Kasowitz, mmoja wa mawakili wake wa binafsi ambaye kwa muda wa miaka 15 amekuwa akishughulikia kesi za masuala yake ya kisheria, kuwemo kwenye kamati ya uchunguzi wa faili la tuhuma za kuwepo uhusiano baina ya timu yake ya kampeni ya uchaguzi na Russia wakati wa kampeni za uchaguzi wa rais wa Marekani mwaka uliopita.

Hatua ya Trump ya kumteua Kasowitz imeonyesha jinsi rais huyo wa Marekani anavyoupa uzito mkubwa uchunguzi unaofanywa dhidi yake kwa hofu kuwa unaweza kumhusisha yeye mwenyewe binafsi na kadhia hiyo. Uchunguzi huo unaongozwa na mkuu wa zamani wa Polisi ya Upelelezi ya nchi hiyo FBI, Robert Mueller.

Rais Trump na Michael Flynn wakati wa kampeni za uchaguzi wa rais

Marc Kasowitz anatazamiwa kuwashirikisha pia mawakili wengine kadhaa katika uchunguzi huo kwa ajili ya kumlinda Trump. 


Maudhui kuu ya uchunguzi huo ni kuingilia Russia uchaguzi wa Marekani na kuwepo uwezekano kwamba rais Trump alikuwa na uhusiano na mawasiliano na maafisa wa Russia wakati wa kampeni za uchaguzi.

Uteuzi wa Kasowitz umefanyika katika hali ambayo Michael Flynn, mshauri wa zamani wa usalama wa taifa wa Rais wa Marekani amekataa kufika mbele ya Kongresi ya nchi hiyo ili kujibu masuali kuhusiana na faili hilo la uchunguzi juu ya kuwepo mawasiliano baina ya timu ya kampeni ya Trump na maafisa wa Moscow wakati ya uchaguzi wa rais Marekani mwaka uliopita wa 2016.../

Chanzo: parstoday.com

No comments:

Post a Comment

Maoni yako