If you need it, we can provide: • USA 24 hours Passport service • Rush and emergency USA passport • Expedited Visa process for U.S. & foreign countries • Document Authentication •Document Legalization..For more information please contact us at: 703-286-7713

http://swahilivilla.blogspot.com/2014/01/mahojiano-na-faria-zam-kuhusu-msaada-wa.htmlKwa kuchangia chochote kile alichonacho kupitia Hilmy Disability Charity Organisation. Wasiliana na Mkurugezi wa Hilmy Disability Charity Organisation. Faria Zam. kwa UK Number ya Simu. 745-501-4372 Au Abou Shatry. U.S.A No' 301-728-3977

 http://www.dickysmallsauto.com/

DICK SMALLS AUTO MOTIVE WE CAN HANDLE ALL OF YOUR REPAIR AND SERVICE NEEDS INCLUDING CALL US NOW!(301) 931-3300. 10111B BACOCON DRIVE,BELTSVILLE,MD 20705


Wednesday, May 10, 2017

Wakorea Kusini wafanya mabadiliko kwa kumchagua Moon Jae-in won Mleberali kuwa rais wao

Habari za hivi punde zinaeleza kuwa, mgombea wa chama cha kileberali Moon Jae-in won, ameshinda katika uchaguzi wa rais nchini Korea Kusini uliofanyika leo. Moon mwenye umri wa miaka 64 ameshinda kwa kupata asilimia 41.4 .

Baada ya ushindi wa Moon Jae-in won, sasa anatazamiwa kumtangaza haraka Waziri Mkuu kwa lengo la kuunda baraza la mawaziri. Uchaguzi wa rais wa mapema nchini Korea Kusini umefanyika leo ikiwa ni baada ya siku 60 kupita tangu alipoondolewa madarakani aliyekuwa rais wa nchi hiyi Bi, Park Geun-hye, kutokana na kashfa za kisiasa na kiuchumi zilizokuwa zikimkabili na ambaye alikuwa mwanamke wa kwanza kuwa rais wa nchi hiyo.

Moon Jae-in won, aliyeshinda uchaguzi wa Korea Kusini

Wagombea katika uchaguzi huo walianza kampeni zao mwezi mmoja uliopita huku wakihitimisha kampeni hizo siku moja kabla ya kuanza kwa shughuli za upigaji kura. Uchaguzi huo umetajwa kuwa na umuhimu mkubwa ambapo changamoto za kiuchumi, masuala ya muungano wa kijeshi na Marekani, kuwekwa nchini humo ngao ya kisasa ya makombora ya Marekani aina ya THAAD na namna ya kukabiliaana na Korea Kaskazini zinazowakabili wananchi zikiwa ndizo zilizoangaziwa sana na wagombea. 

Taarifa iliyotolewa na kanali tatu za Korea Kusini jioni ya leo imemtaja Moon Jae-in won kuwa ndiye aliyeibuka mshindi wa uchaguzi wa leo ingawa awali ilitarajiwa kuwa mshindi angetangazwa kesho Jumatano.

Shughuli ya upigaji kura ilivyokuwa

Jumla ya watu milioni 11 waliotimiza masharti ya kupiga kura walishiriki katika uchaguzi wa mapema uliofanyika siku za Alkhamis na Ijumaa zilizopita kutokana na likizo ya siku tatu. Awali weledi wa mambo walitabiri kujiri mabadiliko mapya katika siasa za rais mpya wa nchi hiyo. 


Jumla ya wagombea 19 wamechuana katika uchaguzi wa leo ingawa ushindani mkali ulionekana kuwa kati ya Moon Jae-in mwanasheria wa masuala ya haki za binaadamu wa chama cha Democrat na Ahn Cheol-soo wa Chama cha Wananchi. 

Hayo yanajiri katika hali ambayo Jumatatu ya jana serikali ya Korea Kaskazini ilionyesha wasi wasi wake mkubwa kwa kurejea madarakani mrengo wa wahafidhina huko Korea Kusini, mrengo ambao ni muitifaki mkubwa wa Marekani.

Pamoja na hali mbaya ya hewa, lakini wananchi wengi walijitokeza kupiga kura

Kabla ya hapo Pyongyang ilikuwa imewataka raia wa nchi hiyo kususia uchaguzi huo ili kutoa pigo kwa Marekani. Kufuatia ushindi wa Moon, inatazamiwa kujiri mabadiliko makubwa katika siasa za Korea Kusini kuihusu Pyongyang. 

Aidha ushindi wa shakhsia huyo ni pigo kwa Washington ambayo ilikuwa ikiwatumia wahafidhina kuishinikiza Pyongyang.

Chanzo: parstoday.com

No comments:

Post a Comment

Maoni yako