If you need it, we can provide: • USA 24 hours Passport service • Rush and emergency USA passport • Expedited Visa process for U.S. & foreign countries • Document Authentication •Document Legalization..For more information please contact us at: 703-286-7713

http://swahilivilla.blogspot.com/2014/01/mahojiano-na-faria-zam-kuhusu-msaada-wa.htmlKwa kuchangia chochote kile alichonacho kupitia Hilmy Disability Charity Organisation. Wasiliana na Mkurugezi wa Hilmy Disability Charity Organisation. Faria Zam. kwa UK Number ya Simu. 745-501-4372 Au Abou Shatry. U.S.A No' 301-728-3977

 http://www.dickysmallsauto.com/

DICK SMALLS AUTO MOTIVE WE CAN HANDLE ALL OF YOUR REPAIR AND SERVICE NEEDS INCLUDING CALL US NOW!(301) 931-3300. 10111B BACOCON DRIVE,BELTSVILLE,MD 20705


Wednesday, June 28, 2017

AFP: Trump ndiye kiongozi anayechukiza zaidi duniani

Matokeo ya uchunguzi wa maoni uliofanywa na taasisi ya Pew unaonesha kuwa, rais wa Marekani Donald Trump ni kiongozi anayechukiwa zaidi duniani ukitoa wananchi wa Russia na utawala wa Kizayuni wa Israel.

Shirika la habari la Ufaransa AFP limeripoti habari hiyo na kuongeza kuwa, kwa mujibu wa uchunguzi wa maoni wa karibuni kabisa uliofanywa na taasisi ya Pew, rais wa Marekani ni kiongozi anayechukiwa zaidi nje ya nchi yake isipokuwa nchini Russia na wakazi wa utawala wa Kizayuni wa Israel. Ukitoa hao, wananchi wa maeneo yote mengine duniani wana imani zaidi na rais wa zamani wa Marekani, Barack Obama, kuliko Donald Trump.

Matokeo ya uchunguzi huo wa maoni uliofanywa na taasisi ya Pew katika nchi 37 duniani yanaonesha kuwa, asilimia 22 tu ya walioshiriki kwenye uchunguzi huo wa maoni ndio walio na imani kwamba Donald Trump anaweza kutoa mchango mzuri katika masuala ya dunia. Ikumbukwe kuwa, wakati anamaliza kipindi chake cha urais nchini Marekani, kiwango cha imani ya walimwengu wa Barack Obama kilikuwa ni asilimia 64.

Kwa mujibu wa uchunguzi huo wa maoni, asilimia kubwa ya watu duniani hawana imani tena na Marekani. Nchi hizo ni pamoja na zile za Amerika ya Latini, Amerika Kaskazini, Ulaya, Asia na Afrika. 

Hisia hizo za kutokuwa na imani na Donald Trump na Marekani yenyewe zinaonekana wazi pia kwa wananchi wa nchi waitifaki wa Marekani za Ulaya, Asia na pia Canada na Mexico.

Mambo mbalimbali yametajwa kuwa sababu ya kutoweka imani ya walimwengu kwa Donald Trump na Marekani yenyewe ikiwa ni pamoja na maamuzi yaliyojaa utata ya rais huyo mpya wa Marekani.

Chanzo: parstoday.com

No comments:

Post a Comment

Maoni yako