If you need it, we can provide: • USA 24 hours Passport service • Rush and emergency USA passport • Expedited Visa process for U.S. & foreign countries • Document Authentication •Document Legalization..For more information please contact us at: 703-286-7713

http://swahilivilla.blogspot.com/2014/01/mahojiano-na-faria-zam-kuhusu-msaada-wa.htmlKwa kuchangia chochote kile alichonacho kupitia Hilmy Disability Charity Organisation. Wasiliana na Mkurugezi wa Hilmy Disability Charity Organisation. Faria Zam. kwa UK Number ya Simu. 745-501-4372 Au Abou Shatry. U.S.A No' 301-728-3977

 http://www.dickysmallsauto.com/

DICK SMALLS AUTO MOTIVE WE CAN HANDLE ALL OF YOUR REPAIR AND SERVICE NEEDS INCLUDING CALL US NOW!(301) 931-3300. 10111B BACOCON DRIVE,BELTSVILLE,MD 20705

Tuesday, June 13, 2017

Amnesty International: Uchunguzi ufanyike kuhusu machafuko ya Kongo

Shirika la Msamaha Duniani (Amnesty International) limeutaka Umoja wa Mataifa kuchunguza machafuko yaliyoukumba mkoa wa Kasai katikati mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo.

Amnesty International imelitaka Baraza la Haki za Binadamu la Umoja wa Mataifa kuunda tume maalumu ya kuchunguza ukiukaji wa haki za kimataifa na zile za binadamu katika mkoa wa Kasai. 

Kamisheni Kuu ya Haki za Binadamu ya Umoja wa Mataifa pia hivi karibuni ilituma tume ya uchunguzi ya kimataifa katika mkoa wa Kasai ili kuweka wazi kuhusu makaburi ya umati 42 yaliyopatikana mkoani humo na vile vile kukiukwa haki za binadamu katika eneo hilo.

Miili iliyotolewa katika makaburi ya umati mkoani Kasai Kongo DR

Nchi wanachama wa Umoja wa mataifa zina muda hadi kufikia tarehe 23 mwezi huu wa kutatua suala hilo. Uhusiano baina ya makabila nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo umeharibika kufuatia kuhamahama jamii na oparesheni zinazofanywa na jeshi dhidi ya wanamgambo wa Kihutu mashariki mwa nchi; huku machafuko na ukosefu wa amani ukiongezeka.

Chanzo: parstoday.com

No comments:

Post a Comment

Maoni yako