If you need it, we can provide: • USA 24 hours Passport service • Rush and emergency USA passport • Expedited Visa process for U.S. & foreign countries • Document Authentication •Document Legalization..For more information please contact us at: 703-286-7713

http://swahilivilla.blogspot.com/2014/01/mahojiano-na-faria-zam-kuhusu-msaada-wa.htmlKwa kuchangia chochote kile alichonacho kupitia Hilmy Disability Charity Organisation. Wasiliana na Mkurugezi wa Hilmy Disability Charity Organisation. Faria Zam. kwa UK Number ya Simu. 745-501-4372 Au Abou Shatry. U.S.A No' 301-728-3977

 http://www.dickysmallsauto.com/

DICK SMALLS AUTO MOTIVE WE CAN HANDLE ALL OF YOUR REPAIR AND SERVICE NEEDS INCLUDING CALL US NOW!(301) 931-3300. 10111B BACOCON DRIVE,BELTSVILLE,MD 20705

Monday, June 12, 2017

AU yasema iko tayari kusuluhisha mzozo wa nchi za Kiarabu

Mwenyekiti wa Umoja wa Afrika amesema yuko tayari kuwa mpatanishi kwenye mgogoro wa nchi za Kiarabu za Ghuba ya Uajemi.

Alpha Conde, ambaye pia ni Rais wa Guinea amemuandikia barua Mfalme Salman wa Saudi Arabia akieleza jinsi alivyosikitishwa na mgogoro huo kati ya Qatar na nchi nyingine za Kiarabu za Ghuba ya Uajemi.

Sehemu ya barua hiyo inasema: "Ningependa kusisizia utayarifu wangu mimi kama Rais wa sasa wa AU na nchi yenye Waislamu wengi, na pia miongoni mwa wanachama waasisi wa Jumuiya ya Ushirikiano wa Kiislamu OIC, kuwa mpatanishi katika mgogoro huo, kwa shabaha ya kuupatia ufumbuzi mzozo huo uliokuja wakati mbaya, miongoni mwa nchi zenye udugu."

Bendera za Saudia na Qatar


Jumatatu iliyopita, Saudi Arabia, Umoja wa Falme za Kiarabu (UAE), Bahrain na Misri zilitangaza kuvunja uhusiano wao wa kidiplomasia na Qatar. Nchi hizo, mbali na mambo mengine, zimedai kuwa serikali ya Doha ni muungaji mkono wa magenge ya kigaidi.

Chad, Niger na Senegal zimewaita nyumbani mabalozi wao mjini Doha kufuatia mgogoro huo. Kadhalika Comoro, Gabon, Mauritania na Djibouti ni katika nchi za Kiafrika zilizofuata kibubusa sera hizo za Saudia za kukata au kupunguza uhusiano wao na Qatar.

Chanzo: parstoday.com

No comments:

Post a Comment

Maoni yako